TANGAZO


Friday, November 1, 2013

Manispaa ya Temeke yatenga zaidi ya sh. milioni 434 kuimarisha usafi

Ofisa Afya Usafishaji toka  Manispaa ya Temeke Ernest Mamuya akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusu hatua mbalimbali zinazochukuliwa na manispaa katika kukabiliana na wachafuzi wa mazingira ikiwa ni pamoja na kutozwa faini isiyopungua 50,000,wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO).katikati ni Afisa Afya Mazingira wa Manispaa hiyo Bw. Willium Muhemu na mwisho ni Afisa Habari wa Manispaa hiyo Bi.Lynn Chawala.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakiwasikiliza wawasilishaji toka Manispaa ya Temeke.
Ofisa Afya Mazingira toka Manispaa ya Temeke Bw. Willium Muhemu akieleza kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) mikakati mbalimbali ya Manispaa hiyo inayotumika katika kuhakikisha wakazi wa manispaa husika wanatekeleza sheria na kanuni za afya zilizoweka ,wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO).Kulia ni Afisa Habari wa Manispaa hiyo Bi. Lynn Chawala. (Picha zote na Hassan Silayo-MAELEZO)


Na Frank Mvungi Maelezo
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke yatenga zaidi ya shilingi milioni 434 katika bajeti ya 2013/2014 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya usafi wa mazingira.
Hayo yamesemwa naAfisa Afya Mkuu wa Manispaa ya Temeke  Bw. Ernest Mamuya leo Jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO.

Alisema manispaa hiyo imeweza kuendesha ukaguzi  katika maeneo ya kutolea huduma kama hoteli na katika makazi ya watu ili kuwabaini wanaochafua mazingira.

Katika kufanikaisha suala la usafi katika manispaa hiyo vifaa vitakavyonunuliwa ni Compactor 1,tela moja la futi 40 kwa ajili ya usafirishaji taka,ununuzi wa mashine 3 za kusafishia barabara,kununua gari 1 la maji taka na kujenga vizimba 3 vya kuhifadhia taka kwa muda.

Ambapo katika kuhakikisha halmashauri inaongeza kiwango cha udhibiti taka na kuboresha hali ya usafi halmashauri imenunua malori mapya 3 aina ya TATA katika bajeti ya 2012/2013 ambayo yaligharimu milioni 324.

Bw. Mamuya alibainisha kuwa manispaa hiyo ina mikakati mbalimbali ikiwemo  kusafisha maeneo muhimu ikiwa ni pamoja na barabara kuu,maeneo ya wazi, masoko,   mifereji  na kuongeza uwezo wa kukusanya taka,kuzihifadhi na kuzisafirisha kwenda dampo.

Alisema  kuwa Mkakati mwingine ni kuelimisha na kuhamasisha jamii ili iweze kuunga mkono na kushiriki katika kuweka mazingira katika hali ya usafi.

Aliongeza kuwa Halmashauri hiyo imefanikiwa kuzuia magonjwa ya milipuko  kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kufuatia mikakati kabambe ya kuhamasisha na kusimamia usafi wa Mazingira katika ngazi ya Kaya na kuigawa halmashauri hiyo katika kanda 5 za ufuatiliji na usimamizi wa usafi wa mazingira ili kurahisisha kazi ya ufuatiliaji na usimamizi wa usafi.

Naye Afisa Habari wa Manispaa ya Temeke Lynn Chawala alisema Manispaa hiyo inatarajia kubadili utaratibu wa kutupa taka dampo    la pugu  na kwenda kutupa Kisarawe II  ambapo ni karibu zaidi hali itakayopunguza gharama za kusafirisha taka.

No comments:

Post a Comment