TANGAZO


Friday, November 1, 2013

Uhuru wa vyombo vya habari hatarini Kenya

 


Wabunge amepitisha mswaada utakaodhibiti vyombo vya habari Kenya
 

Wabunge nchini Kenya wamepitisha mswaada utakaopelekea kuidhinishwa kuundwa kwa jopo maalum litakalodhibiti uhuru wa vyombo vya habari nchini humo.
 
Mswdaa huo utalipa jopo mamlaka kuwaadhibu vikali wanahabari watakaosemekana kuvunja sheria na kukiuka maadili ya utenda kazi kwa kuwatoza viwango vikubwa vya faini.

 
Wamekubali kumtoza faini ya shilingi milioni moja za Kenya mwandishi atakayevunja sheria huku kampuni anayofanyia kazi mwandishi huyo nayo ikitozwa zaidi ya dola laki mbili au shilingi milioni 20 za Kenya kwa kukiuka maadili ya kazi.

Ikiwa mwandishi atakosa uwezo wa kulipa faini hiyo, basi jopo hilo pia lina mamlaka ya kuuza mali yake ili kupata pesa hizo.
Wabunge hao inaarifiwa walipitisha kwa haraka mswaada huo wa kubuni jopo litakaloteuliwa kisiasa ili kuwaadhibu vikali waandishi wataosemekana kukiuka sheria.

Hata hivyo sheria hii inasemekana kuwa moja ya sheria mbaya zaidi za kukandamiza vyombo vya habari kuwahi kushuhudiwa katika historia ya nchi hiyo.

Mswaada huo unaipa serikali mamlaka ya kumwondoa mwandishi wa habari katika sekta hiyo, inaweza kufanya msako katika afisi za vyombo vya habari na kuchunguza akaunti za benki za vyombo hivyo pamoja na zile za waandishi wenyewe.

Jopo hilo linaweza kufanya chochote litakalo kwa sababu linapewa mamlaka makubwa sana na mswaada huo.

Bunge la Kenya linaruhusiwa na katiba kuweka sheria inayodhibiti vyombo vya habari pamoja na kuhakikisha kuwa vinafuata sheria. Lakini katiba hairuhusu serikali hiyohiyo wala wansiasa kusimamia jopo hilo.
Katiba ya Kenya pia hairuhusu serikali kudhibiti vyombo vya habari kwa njia yoyote itakayo.

No comments:

Post a Comment