TANGAZO


Sunday, November 3, 2013

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), yamteua Boniface Wambura kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF

Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura.
 
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemteua Bw. Boniface Wambura kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF. Uteuzi huo ni kuanzia Novemba 2 mwaka huu.

Aidha aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah ameagizwa aende likizo ya malipo hadi atakapomaliza mkataba wake.

Kamati ya Utendaji inaviomba vilabu, vyama vya wilaya, vyama vya mikoa, vyama shiriki na wadau wote kumpa ushirikiano Bw. Boniface Wambura katika utekelezaji wa majukumu yake.

Jamal Malinzi
Rais, Dar es Salaam
 
Novemba 3, 2013

No comments:

Post a Comment