Mtoto wa
Dk. Sengodo Mvungi, Deogratius Mwarabu (kushoto), akiwa na baadhi ya wajumbe wa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Joseph Butiku (katikati) na Profesa Paragamba
Kabudi walipofika Kitengo cha MOI kumjulia hali Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha
NCCR-Mageuzi na Mjumbe wa tume hiyo, ambaye amefikishwa MOI baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana na
kukatwa mapanga.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi,
Dk. Sengodo Mvungi akitolewa katika chumba cha huduma za dharura MOI na
kupelekwa katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam kwa ajili ya
kufanyiwa vipimo.
Wauguzi wakimsaidia kuelekea katika gari la
wagonjwa.
Wauguzi
wakimsaidia kuelekea katika gari la wagonjwa.
Dk. Sengodo Mvungi akipata matibabu ndani ya gari la kubeba wagonjwa wakati akipelekwa Hospitali ya Aga Khan.
Dk. Sengodo
Mvungi akiwa na majeraha kichwani na sehemu za paji la uso. (Picha zote na Habari Mseto Blog)
Na Hapiness
Katabazi
MJUMBE
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini na mhadhiri mwandamzi wa Sheria wa Chuo
Kikuu cha Bagamayo (UB), Dk. Sengondo Adrian Mvungi, saa saba usiku wa kuamkia
leo amevamiwa
na watu wasiyojulikana nyumbani kwake Kibamba nje kidogo ya jiji la Dar es
Salaam na kumcharanga mapanga maeneo ya mwilini mwake ikiwemo sehemu za kichwani
kwa madai kuwa watu hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi walikuwa wakimshinikiza
awapatie fedha na Dk. Mvungi alipowaambia hana fedha ndipo walipoanza
kumcharanga mapanga.
Mtoto mkubwa wa Dk. Mvungi, Dk. Natujwa Mvungi ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Bagamoyo Dar es Salaam, saa nane usiku alimdhibitishia mwandishi wa habari hizi kuwa ni kweli baba yake ambaye aliwahi kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi, lakini kura kwa upande wake hazikutosha na hatimaye aliyekuwa mgombea mwenzie kwa tiketi ya CCM, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, ndiye aliyeshinda na kutangazwa kuwa ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hadi sasa alivamiwa na kujeruhiwa na mapanga na watu wasiyojulikana.
Dk. Natujwa anasema baada ya watu hao kumjeruhi baba yake na kufanikiwa kuondoka, walimchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Tumbi mkoani Pwani, na kupatiwa matibabu ya huduma ya kwanza na kisha kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo alisema kwanza alipokelewa katika eneo la Emergence na kisha saa kumi na moja asubuhi aliingizwa kwenye wodi ya Taasisi ya Mifupa Moi kwa ajili ya kuanza kupewa matibabu.
No comments:
Post a Comment