Nsanii wa muziki wa dansi, Nguza
Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson Nguza 'Papii kocha', katika
chumba cha Mahakama ya Rufaa Tanzania jijini Dar es Salaam leo, kabla ya kuanza
kwa kusikilizwa kwa rufaa yao ya kuitaka mahakama hiyo kupitia upya hukumu
iliyotolewa Februari 10-2010 na mahakama hiyo. Nguza na Papii walihukumiwa
kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji na
ulawiti. (Picha zote kwa hisani ya Francis Dande)
Watu
waliohudhuria mahakamani hapo wakifuatilia kesi hiyo.
Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na
Mwanawe Johnson Nguza au Papii wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Rufaa
Tanzania kabla ya kuanza kwa kusikilizwa kwa rufaa yao, ya kuitaka Mahakama hiyo
kupitia upya hukumu iliyotolewa Februari 10-2010 na mahakama hiyo.
Wakiwa mahakamani leo.
Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na Mwanawe Johnson
Nguza wakiteta jambo na wakili wao, Mabere Marando.
Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na
Mwanawe Johnson Nguza 'Papii' wakiwa na nyuso za furaha wakati wakitoka katika
Mahakama ya Rufaa baada ya majaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania kusikiliza
maombi yao ya kuitaka mahakama hiyo, kupitia hukumu iliyoitoa mwaka
2010.
Nyuso za
matumaini.......
Johnson Nguza 'Papii' akibusu
mkono wake baada ya kuibusu ardhi mara baada ya kutoka mahakamani hapo.
Papii akinyoosha
mkono juu kama ishara ya kumshukuru mungu.
Waandishi wa
habari wakiwa chini wakati wa harakani za kuchukua matukio mahakamani
hapo.
Nguza Vicking 'Babu Seya' akiwa na
Mwanawe Johnson Nguza wakati wakitoka
mahakamani.
No comments:
Post a Comment