Catherine Peter, mkazi wa Sombetini - Arusha, akitoa maelezo kwa Ofisa Tawala wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Lemueli Kileo, namna kifaa cha umeme jua kinavyofanya kazi baada ya kuwa Mtanzania wa 1000 kuunganishwa na nishati hiyo na Kampuni ya Mobisol, umeme huo unaunganishwa kwa wakazi wa maeneo ya vijijini kwa mkopo na kulipa kupitia Vodacom M – PESA. Wanaoshudia kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mobisol, Allan De Mello na Meneja wa Vodacom Mkoa wa Arusha, Philemon Chacha.
Ofisa Tawala Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Arusha, Lemueli Kileo, akiwasha mtambo wa 1000 wa Umeme Jua Nyumbani kwa Catherine Peter ambaye ni Mtanzania wa 1000, kuunganishwa na matumizi ya umeme jua na Kampuni ya Mobisol, umeme huo unaunganishwa kwa wakazi wa maeneo ya vijijini kwa mkopo na kulipa kupitia Vodacom M – PESA. Wanaoshihudia kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mobisol, Allan De Mello na Meneja wa Vodacom Mkoa wa Arusha, Philemon Chacha.
Baadhi ya waandishi wakiwa katika hafla hiyo.
MKUU wa mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo
ametoa wito kwa jamii ya watanzania kujenga utamaduni wa kutumia njia mbadala
za kuzalisha nishati badala ya kuendelea kutegemea serikali kusambaza umeme
kutoka katika gridi ya taifa.
Hayo yamesemwa na Afisa
Tawala Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Arusha, Bwana, Lemueli Kileo wakati akisoma hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa
Arusha katika hafla ya kumkaribisha mteja wa 1,000, aliyefungiwa Mtambo wa sola
wa nyumbani na kampuni ya Mobisol
Mkoani Arusha.
Mkuu huyo wa mkoa amesema
Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kupitia wakala wa Umeme vijijini
REA wameweka malengo kuhakikisha sehemu zote zilizo nje ya gridi ya taifa
zinapata nishati ya umeme.
“Ninawapongeza Vodacom
wakishirikiana na Mobisol kutoka Ujerumani ambao ni wasambazaji wa nishati ya umeme jua kwa njia ya teknolojia
ya simu za mkononi, kwa kuwawezesha Watanzania hasa wa maeneo ya vijijini
wanapata nishati hiyo.” Alisema na kuongeza.
“Ninatoa wito kwa
Watanzania kutumia fursa hii ya kipekee katika kupata nishati kuliko kutegemea
serikali ifikishe Umeme katika maeneo yao kutoka katika gridi ya taifa, hili
litawawezesha watanzania zaidi kupata nishati kiurahisi zaidi.
Kwa upande wake Afisa
Mahusiano wa REA Bi. Jaina Msuya amesema kuwa wakala huyo amefurahia
ushirikiano huo ambao umewezesha watanzania zaidi kupata nishati ya umeme,
Hivyo wao kama wakala wako tayari kushirikiana na wadau mbalimbali kwa kutoa
Ruzuku ambazo zitawawezesha wadau mbalimbali kufikisha umeme vijijini.
“Sisi ni moja ya Taasisi za
serikali zinazotekeleza mpango wa serikali wa matokeo makubwa “Big Result”
hivyo mafanikio haya ni moja ya mafanikio ya utekelezaji wa mpango huo.”
Bibi Catherine Peter, ambaye
ni mteja wa mteja wa 1,000 wa
Mobisol amesema ‘’ Mimi nafurahia sana kuweza kumiliki mtambo wangu wa kwanza
ambao unaotumia nishati ya umeme jua, yaani Solar Home System, Nashukuru sana
mfumo wa kulipia kiasi kidogo kidogo cha pesa kwa mwezi, unaoniwezesha kumudu
kabisa kujipatia mtambo mkubwa wa watts 120, Alisema na kuongeza,
“Natumia mtambo huu wa
solar kuangaza nyumba yangu. Watoto wangu sasa na wajukuu wanaweza kujisomea
usiku bila matatizo ya mwanga na pia nina mpango wa kuanzaisha biashara ya kuchaji
simu za majirani zangu”
Mtambo wa 1,000 uliwashwa
rasmi na Bwana Lemueli Kileo Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Magesa S. Mulongo. Baada
ya mazungumzo na wanahabari waliokuwepo kwenye sherehe pamoja na vingozi waalikwa
kutoka serikalini.
Bwana Thomas Gottschalk,
Meneja Mkuu wa kampuni ya Mobisol amesema: “Tumefanikiwa kubuni mtambo wa bei
nafuu ambao wengi wanaweza kumudu bei yake, ina kidhi mahitaji ya kisasa ya
kiteknologia yenye ubora na ya kudumu.
Kwa mfumo wa kufua nguvu za nishati ya
umeme wa jua au kwa lugha rahisi kuvuna nguvu za Jua.
Mobisol imeweza kutunza
mazingira husika na kuinua hali ya uchumi ya wateja wake sambamba na kuwangaza
majumbani.
“Leo tunasherekea ufungaji
wa mtambo wa 1,000 Tanzania, kesho tunatarajia kwa kiasi kikubwa kuwa uvumbuzi
wa sola itainua na kubandilisha maisha ya mamilioni barani Afrika” alisema
Bwana Gottschalk.
Kwa upande wake, Mkurugenzi
mtendaji wa Vodacom Rene Meza, amesema Vodacom kupitia M pesa wameendelea
kurahisisha maisha ya mamilioni ya Watanzania.
“M–pesa inaendelea kuwa
pendekezo la ufumbuzi wa malipo kwa Watanzania leo na sisi tuliopo Vodacom tutaendelea
kujizatiti kuwapatia wateja wetu bidhaa na huduma bora zinazoendana na mwenendo
wa maisha yao.” Rene Meza
“M-pesa leo imekuwa muundo mbinu ya lazima, yaani imefanya
mapinduzi ya maisha kwa mamilioni ya Watanzania ambao huitegemea kwa huduma za
kifedha ambazo tofauti zinatolewa
na mawakala wetu 50,000 wa M-pesa kote nchini.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Kusambaza Teknolojia ( KAKUTE LTD) kutoka Arusha, Ndugu Livinus S. Manyanga pia aliainisha
kwamba KAKUTE ilikuwa funguo kwa kutoa ushirikiano wa awali wa Wafanyakazi na maendeleo
ya soko la awali ambalo Mobisol walihitaji kwa ukuaji wa biashara yake ndani ya
Arusha tangu ulipoanza mradi wa awali wa majaribio. Aliongeza kwamba KAKUTE
ilichangia kujenga msingi wa upanuzi wa biashara tangu mwanzo kwa uaminifu
uliojijengea na serikali pamoja na taasisi za kusambaza nishati kote Tanzania.
No comments:
Post a Comment