TANGAZO


Wednesday, September 4, 2013

Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru mkoani Dar es Salaam na ukimbizwaji wake wilayani Kinondoni

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki (kulia) akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Pwani na Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania  Hajati Mwantum Mahiza (kushoto) katika uwanja wa ndege wa zamani (Terminal one), leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Hassan Silayo, Eleuteri Mangi, Frank Shija-MAELEZO na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mkuu wa Wilaya ya Mafia Sauda Salum Mtondoo (kulia) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Pwani na Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania  Hajati Mwantum Mahiza (kushoto) kwa ajili ya kuukabidhi Mwenge kwa Mkoa wa Dar es Salaam, katika makabidhiano yaliyofanyika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Barnabas Ndunguru akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mmoja wa wakimbiza mwenge kitaifa kabla ya Mwenge huo kukabidhiwa kwa Mkoa wa Dar es Salaam Kulia ni Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Assah Mwambene.
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mmoja wa wakimbiza Mwenge Kitaifa Zamda John (Tanga) katika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es Salaam. 
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Juma Ali Simai akitoa salamu za shukrani kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Hajati Mwantum Mahiza (aliyevaa Miwani) kabla ya kuukabithi Mwenge huo kwa Mkoa wa Dar es Salaam, katika makabidhiano yaliyofanyika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo(kushoto) akipokea Mwenge wa uhuru kutoka kwa Mmoja wa wakimbiza mwenge kitaifa, katika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Godlease Malisa akisalimiana na Mkimbiza Mwenge Kitaifa Luteni Seperatus Lubinga leo jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Ugavi Anna Chungu na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Titus Mkapa.
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiwa katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ambao umeanza mbio zake leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Godlease Malisa,Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi Anna Chungu, Mkurugenzi  Msaidizi wa Utawala Titus Mkapa, Mkurugenzi wa Idara ya Habari Assah Mwambene, Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala Barnabas Ndunguru, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko,Mkurugenzi wa Sera na Mipango  Joyce Mwakisyala, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana  James Kajugusi, Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Wizara ya Habari Magreth Mtaki, Mkuu wa Kitengo cha Sheria Ester Riwa, na Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu Rose Janeth Bandisa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Said Meck Sadiki akitoa taarifa fupi mara baada ya kupokea Mwege wa Uhuru leo Jijini Dar es Salaam katika uwanja wa ndege wa Terminal one.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2013, Juma Ali Simai, akitoa nasaha zake kwa waathirika wa dawa za kulevya pamoja na wananchi waliofika katika kituo cha vijana hao, Mburahati, Kigogo wakati mwenge huo ulipoanza kukimbizwa wilayani Kinondoni leo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana (kulia), akiwa na Meya wa Manispaa hiyo, Yussuf Mwenda wakati Mwenge wa Uhuru uliposimama kwa muda kwenye kituo cha Vijan waliokuwa wameathirika na dawa za kulevya, Kigogo Mburahati leo wakati Mwenge huo ukiwa katika siku yake ya kwanza ya ukimbizwaji mkoani Dar es Salaam baada ya kumaliza mbio zake mkoani Pwani leo asubuhi  na kisha kukabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa, Said Sadiki, Uwanja wa Ndege wa zamani. 
Mwenge wa Uhuru ukiwa kwenye kituo cha waathirika wa dawa za kulevya, Mburahati, Kigogo leo.
Mwenge wa Uhuru ukiwa kwenye kituo cha waathirika wa dawa za kulevya, Mburahati, Kigogo leo.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2013, Juma Ali Simai, akitoa nasaha zake kwa waathirika wa dawa za kulevya pamoja na wananchi wengine waliofika katika kituo cha vijana hao, Mburahati, Kigogo wakati mwenge huo ulipoanza kukimbizwa wilayani Kinondoni leo.

Vijana waliokuwa wameathirika na madawa ya kulevya wa kituo cha Yovaribe, wakiwa wameshikilia mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati Mwenge wa Uhuru uliliposimama kituoni hapo na kiongozi wa mbio hizo, Juma Ali Simai kutoa nasaha zake.
Luteni Speratus Lubinga, mkimbiza mwenge kutoka mkoani Iringa, akiukimbiza Mwenge wa Uhuru wakati ulipoanza kukimbizwa wilayani Kinondoni jijini leo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Karume, Magomeni Mwembechai, wakiwa wamejitokeza kuupokea mwenge huo.
Mtendaji wa Kata ya Magomeni, Ngaya Swai akisoma risala mbele ya Kiongozi wa mbio za Mwenge, Juma Ali Simai, baada ya Mwenge wa Uhuru, kufika kwenye kata hiyo kwa ajili ya uzinduzi wa Ofisi ya Kata.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana (kulia), akiwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge, Juma Ali Simai (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Dk. Julian Rushaigo wakati wa kusomwa risala hiyo.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2013, Juma Ali Simai, akikata utepe ili kuzindua jengo la Ofisi za Kata ya Magomeni, Dar es Salaam leo. 

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2013, Juma Ali Simai, akikata utepe ili kuzindua jengo la Ofisi za Kata ya Magomeni, Dar es Salaam leo. 
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2013, Juma Ali Simai, akifunua pazia ili kuzindua jengo la Ofisi za Kata ya Magomeni, Dar es Salaam leo. 
 Hili ni jiwe la msingi la Ofisi ya Kata hiyo ya Magomeni.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Ali Hassan Mwinyi wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa jengo hilo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Ali Hassan Mwinyi wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa jengo hilo.
Wasanii wa kikundi cha Albino Arts, wakitumbuiza wakati Mwenge wa Uhuru ulipofika Shule ya Sekondari ya Magomeni jijini leo.

No comments:

Post a Comment