1. Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Valentine Msusa akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu maboresho ya
makusanyo ya mapato ya Serikali kwenye sekta ya Misitu, wakati wa mkutano
uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari, Maelezo leo, jijini Dar es Salaam. Kulia
ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo, Frank Mvungi.
Wakala
wa Huduma ya Misitu Tanzania katika kutekeleza mpango wa Matokeo Makubwa sasa
(Big Results Now), pamoja na Sera ya Misitu ambayo inasisitiza katika
kuhakikisha uendelezaji endelevu wa misitu, umefanya maboresho katika maeneo
mbalimbali ili kuhakikisha mapato ya Serikali yanaongezeka na kuongeza udhibiti
wa uvunaji na ukusanyaji wa mapato. Maeneo yaliyofanyiwa maboresho ni pamoja
na;
- Kufanya mapitio ya bei ya mazao
ya misitu,
- Kufanya mapitio ya Mwongozo wa
uvunaji endelevu wa misitu wa mwaka 2007,
- Uuzaji wa miti ya Misaji (Teak)
kwa njia ya mnada na
- Kuimarisha ulinzi katika vizuia na kusitisha ukusanyaji wa maduhuli katika vizuia hivyo.
Kuanzia
tarehe 14/09/2013 ukusanyaji wa tozo, faini na malipo yo yote ya fedha kwenye
vizuia umezuiliwa. Mazao yoyote
yatakayokutwa sio halali au nyaraka zake zina mapungufu gari litazuiwa katika
kizuia na mhusika atapaswa kulipa faini katika vituo vilivyoteuliwa kufanya
kazi hiyo. Mazao yaliyozidi au kutokuwa na nyaraka halali yatateremshwa na
kutaifishwa.
Katika
kufanya maboresho hayo wakala umefanya yafuatayo:
(i)
Mapitio
ya bei ya mazao ya misitu
Bei za mazao ya misitu zitapandishwa kwa kuzingatia utafiti
uliofanywa na mshauri mwezeshaji ambaye amezingatia
·
gharama
za uzalishaji wa miche ya miti hadi kufikia hatua ya kuvunwa,
·
kupanda
kwa gharama za huduma na vifaa vya uzalishaji na kiwango cha ubadilishaji wa
fedha ya Tanzania, na
·
Kupanda
kwa Gharama za vibarua na wafanya biashara wanaotoa huduma katika mashamba ya
miti
Maboresho hayo yatapunguza hasara ambayo Serikali
inapata kutokana na kuuza mazao ya misitu kwa bei ya chini.
(ii)
Kufanya
mapitio ya Mwongozo wa Uvunaji Endelevu wa Misitu wa mwaka 2007.
Maeneo yaliyoboreshwa ni pamoja na
·
Kuandaa
Miongozo miwili tofauti iliyotayarishwa kwa ajili ya Mashamba ya Miti na Misitu
ya Mikoko na ule wa Misitu ya Asili.
·
Kuboresha
takwimu za hali ya misitu hapa nchini na
·
kuweka
Masharti ya viwanda vya kuchakata mazao ya misitu kama ilivyoainishwa katika
Sheria ya Misitu ya mwaka 2002.
Mwongozo huu
unawaelekeza wadau na wananchi kwa ujumla juu ya;
- utaratibu wa kuvuna,
- usimamizi na kufanya biashara
ya mazao ya misitu,
- masharti ya kuanzisha viwanda
vya kuchakata mazao ya misitu,
- masharti ya kufanya biashara ya
mazao ya misitu ndani na nje ya nchi,
- nyaraka mbalimbali
zinazokubalika kisheria wakati wa kuvuna,
- kusafirisha na kufanya biashara
ya mazao ya misitu,
- utaratibu wa namna vijiji vinavyopakana na misitu vitakavyonufaika na misitu inayowazunguka.
(iii)
Uuzaji
wa Miti ya Misaji (Teak) kwa Njia ya Mnada
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, ulianza kutekeleza
uuzaji wa mazao ya misitu kwa mnada mwaka 2012/2013. Zoezi hili limetekelezwa
kwenye Mashamba ya miti ya Misaji (Teak) yaliyopo Longuza, Mtibwa na Rondo. Matokeo
mnada huo yalikuwa mazuri na tulipata
ongezeko la bei kwa asilimia (66%) kwa
kila mita ya ujazo. Hivyo uzoefu huu unaonyesha kuwa uuzaji wa miti kwa njia ya
mnada unaleta matokeo makubwa kuliko njia nyingine.
Pamoja na faida hiyo imeonekana mnada una gharama ndogo
za kiutawala, uwazi, na unatoa fursa kwa wavunaji wadogo na wakubwa kushiriki. Aidha,
zoezi la uaandaaji wa mnada unachukua muda mfupi. Katika Mashamba ya miti laini
(softwood) ya kupandwa, maandalizi ya utaratibu wa mauzo, yatazingatia uzoefu wa
mnada wa miti ya misaji na uamuzi utafanyika baada ya kufanya utafiti wa
kutosha.
(iv)
Kuimarisha Ulinzi Katika Vizuia Na
Kusitisha Ukusanyaji Wa Maduhuli Katika Vizuia Hivyo.
Wakala
umeamua kusitisha ukusanyaji wa tozo, faini, na malipo yoyote ya fedha kwenye Vizuia vya ukaguzi wa mazao ya misitu na
hivyo vitafanya kazi ya ukaguzi tu ili kuhakiki kama mazao yanayosafirishwa
yamelipiwa ushuru na tozo nyingine na
kama yana nyaraka halali
No comments:
Post a Comment