Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dk. Charles Musonde, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa Shirikisho la Mabaraza ya Upimaji na Tathmini ya Elimu Afrika (AEAA), utakaofanyika jijini Arusha kuanzia Agosti 12 hadi 16, mwaka huu. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa baraza hilo, Daniel Mafie. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dk. Charles Musonde, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa Shirikisho la Mabaraza ya Upimaji na Tathmini ya Elimu Afrika (AEAA), utakaofanyika jijini Arusha kuanzia Agosti 12 hadi 16, mwaka huu. Kushoto kwake ni Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa baraza hilo, Daniel Mafie.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dk. Charles Musonde, alipokuwa akizungumza nao kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa Shirikisho la Mabaraza ya Upimaji na Tathmini ya Elimu Afrika (AEAA), utakaofanyika jijini Arusha kuanzia Agosti 12 hadi 16, mwaka huu.
Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa baraza hilo, Daniel Mafie, akizungumza katika mkutano huo leo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dk. Charles Musonde.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dk. Charles Musonde, alipokuwa akizungumza nao kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa wa Shirikisho la Mabaraza ya Upimaji na Tathmini ya Elimu Afrika (AEAA), utakaofanyika jijini Arusha kuanzia Agosti 12 hadi 16, mwaka huu.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa katika mkutano huo, wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dk. Charles Musonde, alipokuwa akizungumza nao kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa Shirikisho la Mabaraza ya Upimaji na Tathmini ya Elimu Afrika (AEAA), utakaofanyika jijini Arusha, kuanzia Agosti 12 hadi 16, mwaka huu.
Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dk. Charles Musonde, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa Shirikisho la Mabaraza ya Upimaji na Tathmini ya Elimu Afrika (AEAA), utakaofanyika jijini Arusha kuanzia Agosti 12 hadi 16, mwaka huu. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa baraza hilo, Daniel Mafie.
Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dk. Charles Musonde, akijibu maswali ya waandishi wa habari kwenye mkutano huo jijini leo.
Na Eben-Ezery Mende
TANZANIA mwaka huu itakuwa mwenyeji wa mkutano wa Shirikisho la Mabaraza ya Upimaji na Tathmini ya Elimu Afrika ambapo mkutano huo utafanyika, Agosti 12 hadi 16 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania, Dk. Charles Msonde mkutano huo utafanyikia mkoani Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, Dk. Msonde alisema mkutano huo ni wa 31 tangu kuanzishwa shirikisho hilo (AEAA) na kufanyika Tanzania mwaka huu itakuwa awamu ya tano.
Alisema mkutano huo utafunguliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi ambapo viongozi mbalimbali wa Serikali na wadau wa elimu watashiriki.
Dk. Msonde alisema zaidi ya washiriki 400 wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo ambapo kubwa litakalojadiliwa ni mwenendo wa elimu ya Afrika na kubadilishana uzoefu wa kutathmini na kupima elimu kwa nchi za Afrika.
Alisema baadhi ya washiriki wa mkutano huo watatoka Ulaya, Marekani na Asia. Tanzania ilikuwa mwenyeji wa mkutano kama huo kwa mara ya kwanza mwaka 1983, mara ya pili 1987 kisha 1992 na mwaka 2002.
No comments:
Post a Comment