Kaimu Mkurugenzi Mkuu kutoka Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi
Serikalini (GEPF) Festo Fute akiongea na waandishi wa Habari kuhusu mpango wa
hiari wa kujiwekea akiba ya uzeeni (VSRS) kwa watu wote ili kupambana na majanga
mbalimbali, Katika mkutano uliofanyika leo ukumbi wa Idara ya Habari leo Jijini
Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa. (Picha na Frank
Mvungi-MAELEZO)
TAARIFA
KWA UMMA KUHUSU MFUKO WA AKIBA GEPF
1.0
UTANGULIZI
Mfuko
wa Akiba GEPF ulianzishwa chini ya sheria Namba 51 ya mwaka 1942 iliyofanyiwa
marejeo mwaka 2002 (Re 2002). Madhumuni ya Mfuko hapo awali ilikuwa kutoa huduma
ya hifadhi ya jamii kwa watumishi wa serikali kuu ambao utumishi wao ilikuwa si wa masharti ya kudumu na malipo ya
pensheni. Mfuko huu toka kuanzishwa mwaka 1942 ulifanya kazi zake chini ya
Wizara ya Fedha mpaka kufikia mwaka 2004 ambapo Mfuko ulipata Bodi yake na
Menejimenti na kuanza kufanya kazi kama taasisi ya umma inayojitegemea.
2.0
MAGEUZI
KATIKA SEKTA YA HIFADHI YA JAMII
Sekta
ya hifadhi ya jamii imepitia mageuzi mbalimbali katika kipindi cha muongo mmoja
uliopita. Mageuzi hayo yamechochewa na Sera ya Taifa ya Hifadhi ya jamii ya
mwaka 2003. Sera hiyo imeainisha changamoto mbalimbali za sekta. Matokeo ya
sera hiyo ni kuanzishwa kwa Mamlaka ya Kusimamia na Kuratibu Sekta ya Hifadhi
ya Jamii kwa sheria Na. 8 ya mwaka 2008.
Sheria hiyo imekuja na mageuzi makubwa katika sekta ya hifadhi ya jamii ambapo
pamoja na mambo mengine imefungua milango kwa Mifuko iliyopo nchini kusajili
wanachama bila mipaka kama ilivyokuwa hapo awali. Lakini pia sheria hiyo
inaruhusu kuwafikia watu wote wenye
uwezo wa kuzalisha kipato bila kujali aina ya ajira.
3.0
WANACHAMA
WA MFUKO
GEPF
ni Mfuko unaoendeshwa kwa mfumo wa akiba tofauti na Mifuko mingine
inayoendeshwa kwa mfumo wa bima. Hivyo wanachama wa GEPF wanatokana na
waajiriwa wote wanaofanya kazi kwa mikataba na wale wote ambao ajira zao
hazikidhi kulipwa pensheni. Mageuzi ya sekta yametoa fursa ya kusajili
watumishi bila mipaka, hivyo waajiriwa wote walio katika masharti ya mikataba
wanaweza kujiunga na Mfuko huu, Lakini pia wale wote waliojiajiri wenyewe
wanaweza kujiunga na GEPF chini ya mpango maalum ujulikanao kama Mpango wa
Hiari wa Kujiwekea Akiba ya Uzeeni maarufu kama VSRS.
Idadi
ya wanachama imeongezeka kutoka wanachama 30,227 mwaka 2008/09 hadi kufikia
wanachama 60,030 mwezi Juni, 2013 hii ni kutokana na jitihada za Mfuko kuhakikisha watu wote wenye
uwezo wa kuweka akiba wanafanya hivyo.
Jedwali Na. 1: Ongezeko la idadi ya
wanachama kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita
Mwaka
|
2008/09
|
2009/10
|
2010/11
|
2011/12
|
2012/13
|
Wanachama
|
30,227
|
35,279
|
41,879
|
52,670
|
60,030
|
Chati Na. 1: Ongezeko
la wanachama katika kipindi hicho
4.0
MAENDELEO
YA MFUKO
Maendeleo
ya Mfuko hupimwa kwa kuangalia ongezeko la thamani ya Mfuko. Kwa kipindi cha
miaka mitano iliyopita Mfuko umeweza kukua kwa kasi kubwa, hii inatokana na
ongezeko la michango ya wanachama na kufanya uwekezaji wenye tija. Thamani ya
Mfuko imeongezeka kutoka Sh. 72.55 bilioni mwaka 2008/09 hadi kufikia kiasi cha
Sh. 198.30 bilioni mwezi Juni, 2013.
4.1 Jedwali
Na. 2: Ongezeko la thamani ya Mfuko kwa kipindi cha miaka mitano
Mwaka
|
2008/09
|
2009/10
|
2010/11
|
2011/12
|
2012/13
|
Thamani (Bilioni)
|
72.55
|
91.28
|
119.40
|
154.50
|
198.30
|
Chati Na. 2: Ongezeko la thamani ya Mfuko
4.2 Uwekezaji wa fedha za wanachama
Ili
kulinda thamani ya michango ya wanachama Mfuko hufanya uwekezaji katika maeneo
mbalimbali yaliyo salama na yanayotoa faida kubwa. Mfuko huwekeza kwenye Amana za Serikali, Makampuni yaliyo
orodheshwa kwenye soko la mitaji (DSE),
Uwekezaji wa muda maalum kwenye mabenki ya biashara, Mikopo, Hati
fungani na Majengo. Vitegauchumi vya Mfuko viliongezeka kutoka Sh. 64.94
bilioni mwezi Juni, 2009 hadi kufikia Sh. 179.68 bilioni mwezi Juni, 2013.
Vilevile mapato yaliongezeka kutoka Sh. 5.48 bilioni mwezi Juni, 2009 hadi
kufikia Sh. 18.25 bilioni mwezi Juni, 2013.
Jedwali Na. 3: Ongezeko la mapato ya
uwekezaji kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita
Mwaka
|
2008/09
|
2009/10
|
2010/11
|
2011/12
|
2012/13
|
Vitegauchumi
(Bilioni)
|
64.94
|
82.47
|
101.29
|
137.75
|
179.68
|
Mapato (Bilioni)
|
5.48
|
7.69
|
9.81
|
11.54
|
18.25
|
Chati Na. 3: Ongezeko la
mapato ya uwekezaji katika asilimia (%)
4.3 Ongezeko la michango ya wanachama
Katika
kipindi cha miaka mitano iliyopita michango ya wanachama imekuwa inaongezeka
kwa kasi. Hii inasaidia katika ukuaji wa Mfuko moja kwa moja lakini pia
kuongeza mapato yatokanayo na uwezekezaji.
Jedwali Na. 4: Ongezeko la michango ya
wanachama kwa kipindi cha miaka mitano
Mwaka
|
2008/09
|
2009/10
|
2010/11
|
2011/12
|
2012/13
|
Mapato (Bilioni)
|
13.79
|
16.32
|
25.71
|
30.15
|
37.29
|
Chati Na. 4: ongezeko la michango ya wanachama katika asilimia (%)
5.0
ULIPAJI
WA MAFAO KWA WANACHAMA
Mfuko
wa GEPF hulipa mafao ya mkupuo (lump-sum) kwa wanachama wake kulingana na aina
ya ajira zao. Wengi wa wanachama wa mfuko huu ni wafanyakazi wa mikataba, hivyo
pindi wamalizapo mikataba yao hulipwa mara moja. Ulipaji wa mafao huzingatia
michango kutoka kwa mwanachama na mwajiri pamoja na faida anayopewa mwanachama
kila mwaka kutokana na mapato ya uwekezaji. Katika kipindi cha mwaka wa fedha
2012/13 jumla ya kiasi cha TZS. 5.25
Bilioni kililipwa kwa wanachama ikiwa ni mafao yao.
6.0
MPANGO
WA HIARI WA KUJIWEKEA AKIBA YA UZEENI (VSRS)
Hii
ni Skimu maalum ambayo imebuniwa mwaka 2009 ili kutoa fursa kwa watu wote
kuweka akiba ambayo itawasaidia kupambana na majanga mbalimbali ikiwemo uzee.
Mpango huu ni matokeo ya mageuzi katika sekta ambayo yanamtaka kila mtu mwenye
uwezo wa kuzalisha kipato anaweza kujiunga na Hifadhi ya Jamii. Kupitia Skimu
hii kila mtu anaweza kujiunga, awe mkulima, mjasiliamali, sekta ya usafiri na
makundi mengine.
GEPF
ulikuwa Mfuko wa kwanza kuanzisha Skimu ya aina hii hivyo mafanikio
yaliyofikiwa kwenye Skimu hii ni makubwa sana ukilinganisha na Mifuko mingine.
Skimu hii imeundwa kwa kuzingatia mazingira rafiki ya makundi yote ya
uzalishaji. Kwa mfano uchangiaji wa michango haujali kiwango maalum wala muda
maalum, ni moja ya muundo unaomwezesha kila mtu kwa kipato chake kuweza
kujiwekea akiba. Wanachama wanawekewa faida kila baada ya miezi sita pia wana
fursa ya kutumia mpaka 50% ya akiba yao pindi wanapopata dharura.
6.1 Mafanikio katika Skimu ya Hiari (VSRS)
Toka
kuanzishwa kwake Novemba, 2009 Skimu hii imefanikiwa kusajili wanachama 18,700 kufikia Juni, 2013. Jumla
ya akiba za wanachama zilifikia kiasi cha TZS. 3.05 Bilioni katika kipindi hicho.
Jewali Na. 5: Mchanganuo wa
usajili wa wanachama wa VSRS hadi Juni, 2013;
Mwaka
|
Nov. 09 – Jun. 10
|
2010 - 2011
|
2011-2012
|
2012-2013
|
JUMLA
|
Usajili
|
1,644
|
4,911
|
6,688
|
5,457
|
18,700
|
Chati Na. 5: Usajili wa wanachama
wa VSRS
Jedwali Na. 6: Mchanganuo wa
michango ya wanachama wa VSRS hadi Juni, 2013
Mwaka
|
Nov. 09 – Jun. 10
|
2010 - 2011
|
2011-2012
|
2012-2013
|
JUMLA
|
Michango (Milioni)
|
59.48
|
311.44
|
840.76
|
1,839.12
|
3,050.80
|
Chati Na. 6: Mchanganuo wa michango wa wanachama wa VSRS;
6.2 Mgawanyiko wa wanachama kisekta
Katika
jumla ya wanachama 18,700 walisajiliwa mpaka kufikia June, 2013 mgawanyiko wao
kisekta ni kama inavyoonekana kwenye jedwali namba 7.
Jedwali
Na. 7: Mgawanyiko wa wanachama wa VSRS kisekta
Sekta
|
Biashara
|
Kilimo na ufugaji
|
Usafirishaji
|
Waajiriwa
|
JUMLA
|
Wanachama
|
7,480
|
6,545
|
1,683
|
2,992
|
18,700
|
Chati Na. 7: Mgawanyiko wa wanachama wa VSRS kisekta
7.0
CHANGAMOTO
Pamoja
na mafanikio yaliyoainishwa hapo juu, Mfuko umekuwa unakabiliana na changamoto
mbalimbali ambazo ni;
i)
Kupitwa na wakati kwa sheria inayoongoza
Mfuko ambayo inafanyiwa mapitio hivi sasa
ii)
Ufahamu mdogo wa watu kuhusu Mfuko
No comments:
Post a Comment