TANGAZO


Saturday, August 31, 2013

Cheka amdunda Phill William wa Marekani mkanda wa Ubingwa wa Dunia WBF

 Pambano la utangulizi kati ya Allan Kamote (kushoto), aliyekuwa akikwaruzana na Deo Njiku. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogger.com).
 Allan Kamote (kushoto) na Deo Njiku wakiwa kazini usiku huo.
Bondia Chupaki Chipindi (kushoto), akiwindana na Alphonce Mchumiatumbo katika mpambano uliosisimua sana ukumbini hapo.
 Bondia Chupaki Chipindi (kulia), akikwepa konde la mpinzani wake, Alphonce Mchumiatumbo.
 Hapa wakivaana kila mmoja akijihami asiadhibiwe na makonde ya mwenzake.
 Chupaki Chipindi (kushoto), akishikana na mpinzani wake, Alphonce Mchumiatumbo.
 Chupaki Chipindi (kushoto), akikwepa konde la mpinzani wake, Alphonce Mchumiatumbo.
Bondia Alphonce Mchumiatumbo, akimdondosha chini mpinzani wake, Chupaki Chipindi, huku naye akipepesuka, akitaka kumdondokea, wakati wa pambano la utangulizi kabla ya Cheka na William hawajapanda ulingoni kuwania mkanda wa dunia wa WBF ukumbini hapo. Mchumiatumbo alishinda kwa TKO ya raundi ya tano.
Hapa mabondia hao wakitoana ngeu kutafuta ushindi wa mpambano wao huo.
Mabondia hao, waliendelea kupambana hadi raundi ya tano, ilipowadia na hapo Chupaki Chipindi, akasalimu amri akiokolewa asipate kipigo zaidi.
 Mchumiatumbo akitangazwa kuwa mshindi wa mpambano huo.
Mabosi wa TBL wakiwa na washikaji wao wakifuatilia mpambano wa ngumi kati ya Mada Maugo na Francis Miyeyusho.
Mada Maugo na mpizani wake wakitafutana kabla ya kurusha makonde ili kujitafutia ushindi kwa pamzani wake huyo. 
Mada Maugo akimpiga konde la mkono wa kulia mpinzani wake, Thomas Mashali wakati wa mpambano wao wa kuwania ubingwa wa Shirikisho la Ngumi barani Africa (IBF Africa Cahmpionship), ambapo Mashali alimshinda mpinzani wake huyo kwa pointi.
Waziri Mukangala akizungumza na mabondia Francis Cheka (kulia) na William wa Marekani (kushoto) kabla ya kuanza kwa pambano lao la kuwania mkanda wa Shirikisho la Ngumi (WBF).
Waziri Mukangala akipiga ngumi kwenye mkono wa Francis Cheka kabla ya kuanza mpambano wao huo.
Mmoja wa Raia wa Marekani akiimba wimo wa Taifa hilo kabla ya kuanza pambano lao hilo.
Cheka akimpiga ngumi ya paji la uso mpinzani wake huyo.
Cheka akimpiga ngumi ya mbavu mpinzani wake huyo.
Cheka akijihami na gumi kutoka kwa mpinzani wake huyo.
Mabondia Cheka na William wakisomana kabla ya kurusha ngumi kwa mwenzake.
Mabondia Cheka na Phill William wakiangaliana kabla ya kila mmoja kumrushia konde mwenzake katika mpambano huo.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk, Fenella Mukangara akiwa na Waziri Mathayo na Mkurugenzi wa Michezo, Leonard Thadeo wakiangalia mpambano wa Cheka na William.
Cheka na William kutoka Marekali wakiingiana mwilini ili kila mmoja aweze kujihami kwa mwenzake.
Bondia William wa Marekani akikwepa ngumi iliyotupwa na mpinzani wake, Francis Cheka katika mpambano huo.
Cheka (kulia) na mpinzani wake, wakijihami kila mmoja akimhofia  mwenzake katika mpambano huo.
Cheka (kulia), akimwangalia mpinzani wake ili aweze kupitisha makonde usoni mwake.
Bingwa wa zamani wa dunia wa mchezo huo, wa Afrika Kusini, bondia Francois Botha (kulia), akitetea jambo na msimamizi wa mpambano huo.
Cheka akimtupia konde la mkono wa kushoto mpinzani wake, William wa Marekani katika kuwania mkanda huo.
Cheka na William wakitafutana, kila mmoja akiangalia sehemu ya kutupa konde lake usoni kwa mwenzake.
Wlliam akifunguliwa vitambaa alivyokuwa amevifunga kwenye mkonowake wakati wa pambanano hilo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Fenella Mukangala, akimvisha mkanda wa Ubingwa wa dunia wa Shirikisho la Ngumi Ulimwenguni (WBF), Francis Cheka baada ya kumdunda kwa pointi bingwa wa dunia aliyekuwa akiushikilia mkanda huo, Phill William wa Marekani katika mpambano wa raundi 12, uliofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Fenella Mukangala, akimvisha mkanda wa Ubingwa wa dunia wa Shirikisho la Ngumi Ulimwenguni (WBF), Francis Cheka baada ya kumdunda kwa pointi bingwa wa dunia aliyekuwa akiushikilia mkanda huo, Phill William wa Marekani katika mpambano wa raundi 12, uliofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Mashabiki wa bondia Francis Cheka, wakimshangilia baada ya kumtwanga William na kunyakua mkanda wa ubingwa wa dunia wa Shirikisho la Ngumi Ulimwenguni (WBF) kwa uzito wa middle (76kgs), ukumbini hapo usiku wa kuamkia leo.
Mashabiki wa bondia Francis Cheka (katikati), wakiwa wamemzunguka baada ya kumtwanga William na kunyakua mkanda wa ubingwa wa dunia wa Shirikisho la Ngumi Ulimwenguni (WBF) kwa uzito wa middle (76kgs), ukumbini hapo usiku wa kuamkia leo.
Cheka akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushinda pambano hilo, usiku wa kuamkia leo. jijini Dar es Salaam.

Na Magendela Hamisi
BONDIA Francis  Cheka ameudhihirishia ulimwengu kuwa  Tanzania ni miongoni mwa nchini zinazofanya vizuri katika tasnia ya masumbwi baada ya kumtandika Phil Williams wa Marekani na kutawazwa kuwa bingwa wa dunia wa mkanda wa WBF.

Cheka maarufu kwa jina la SMG alimchapa bondia huyo kutoka taifa kubwa la Marekani juzi katika Ukumbi Diamond kwa pointi katika pambano la raundi 12 lililokuwa na upinzani mkubwa, huku Waziri wa Habari Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mkangala akiwa mgeni Rasmi

Pambano hilo lilianza kwa kila bondia kusoma mbinu za mwezake na ilipofika raundi ya tatu Cheka alianza kuonesha  makali yake baada ya kutupa makonde mazito dhidi ya mpinzani wake na kumwangusha katika raundi ya nne.

Mashabiki waliofurika katika ukumbi huo walilipuka kwa shangwe baada ya Cheka kumwangusha William hali iliyompa ujasiri Cheka kuendelea kufanya vizuri licha ya kupata upinzani mkubwa kutoka kwa mmrekani huyo mwenye rekodi nzuri katika masumbwi.

Ilipofika raundi ya saba mabondia hao walitupiana makonde kwa zamu hali ilioonesha mchezo huo kuwa mgumu kwa pande zote lakini mashabiki waliofurika katika ukumbi huo waliendelea kushangilia kwa nguvu hadi raundi 12.

Baada ya raundi 12 za pambano hilo la uzito wa kati la ubingwa wa dunia wa WBF lililochezeshwa na mwamuzi kutoka Afrika kusini, Drake Ribbinck majaji watatu walitoa alama zilizotangaza Cheka kuwa bingwa mpya wa mkanda huo.

Jaji namba moja kutoka nchini Afrika Kusini, Eddie Marshall alitoa alama 119 kwa 115, jaji namba mbili alitoa alama 119 kwa 108 na jaji namba tatu Mtanzania John Chagu alitoa alama 117 kwa 111, kwa pamoja wakimpa ushindi Cheka.

Mshehereshaji wa pambano hilo Daniel Kijo alipotangaza majibu ya pambano hilo na Cheka kutangazwa mshindi na kuwa bingwa wa mkanda wa dunia WBF katika uzito wa kati mamia ya mashabiki waliofurika katika ukumbi walilipuka kwa shangwe.

Baada ya mchezo huo, Cheka alikiri kupata upinzani kutoka kwa Williams na kuwashukuru Watanzania kwa kumuunga mkono huku akitoa mwito kwa mapromota kujitokeza kusaidia mchezo huo ambao una changamoto nyingi.

Kabla ya pambano hilo kulikuwa na mapambano manne ya utangulizi ambapo katika pambano la kwanza bondia Ibrahim Class 'King Class Mawe' alimchapa kwa pointi Simba Watunduru, Allain Kamote kutoka Tanga alichakaza kwa pointi Deo Njiku wa Morogoro.

Pia Alphonce Mchumiatumbo akamtwanga kwa KO katika raundi ya tano bondia Chupa Chipindi na Thomas Mashali 'Simba Asiyefugika' akimng'ota kwa pointi Mada Maugo na kutawazwa kuwa bingwa wa  mkanda wa  WBF Afrika katika pambano la raundi 10.

Licha ya pambano kufana kutokana na mabondia wa Tanzania kutawazwa kuwa mabingwa, liliingia dosari baada ya mchezo wa kwanza wa utangulizi kumalizika wanasumbwi kugoma kuingia ulingoni hadi walipwe fedha zao.

Kutokana na hali hiyo kujitokeza na kuonesha taswira mbaya katika mchezo huo na kuonekana kama wa kihuni baadhi ya baadhi ya viongzi wa kiserikali walioudhuria pambano hilo walitoa matamko yao akiwemo Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dk. David Mathayo.

Moja ya tamko walililotoni ni kutaka vyombo husika kuwachuliwa hatua kali waandaji wa pambano hilo kutokana na dosari zilizojitokeza kwani imelitoa doa taifa hali iliyodhohirisha kulikuwa hakukuwepo kwa maandaliz ya kutosha.

No comments:

Post a Comment