TANGAZO


Saturday, August 17, 2013

Kiprotich ashinda dhahabu Moscow


Kiprotich
Stephen Kiprotich wa Uganda akishangilia ushindi wake
Stephen Kiprotich wa Uganda alinyakua medali ya dhahabu ya mbio za marathon katika michuano ya ubingwa wa riadha wa dunia mjini Moscow,na kwa mara nyingine tena kuvipiku vikosi vizito vya Ethiopian na Kenya.
Kiprotich alishinda mbio hizo kwa muda wa saa 2 dakika 09 na sekunde 51. Waethiopia Lelisa Desisa na Tadese Tola walishikilia nafasi ya pili na ya tatu.
Hii ni medali ya pili ya dhahabu ya Uganda katika mashindano ya ubingwa wa dunia baada ya Dorcus Inzikuru kushinda mbio za mita 3000 kuruka maji na viunzi mnamo mwaka 2005 mjini Helsinki.
Kiprotich mwenye umri wa miaka 24-aliwashangaza wengi aliposhinda mbio za marathon za michezo ya Olympiki ya London mwaka jana. Lakini mjini Moscow alionekana kujipanga vizuri akichuana na Waethiopia na Wakenya hadi kuwashinda nguvu na kunyakua medali yake ya pili ya dhahabu katika michezo mikuu ya kimataifa.

No comments:

Post a Comment