Msimu wa Ligi Kuu ya soka ya England umeanza kwa kishindo kwa Aston Villa kuwashtua Arsenal kwa mabao 3-1 katika uwanja wa Emirates.
Arsenal ndio waliofungua mlango katika dakika ya 6 kupitia Olivier Giroud. Lakini mabao mawili ya Christian Benteke kwa mikwaju ya penati yaliwakatisha tamaa mashabiki wa Arsenal.
Bao la tatu la Villa limefungwa na Antonio Luna.
Wengine walioshinda ugenini ni Fulham walioifunga Sunderland bao moja kwa bila na Southampton waliilaza West Bromwich pia kwa bao moja kwa bila liliofungwa na Rickie Lambert. Liverpool iliibuka na ushindi wa chupu chupu wa bao moja kwa bila dhidi ya Stoke City liliofungwa na Daniel Sturridge, goli la kwanza kufungwa msimu huu.
Mlinda lango Mignolet aliiokoa penalti katika dakika za mwisho za mchezo huo. Westham United waliwakaribisha Cardiff City katika ligi kuu kwa kuwafunga mabao mawili kwa bila. Norwich City ilitoka sare mawili kwa mawili na Everton.
No comments:
Post a Comment