Baadhi ya wanawake wajasiriamali wadogowadogo wa Tarafa ya
Matombo Morogoro vijijini wakipatiwa elimu na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania
hawapo pichani,kabla ya kupatiwa mikopo yao ya pesa isiyokuwa na riba ya zaidi
ya shilingi Milioni 327 iliyotolewa na Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa “MWEI”.mikopo hiyo
inawawezesha wanawake wajasiriamali wadogowadogo nchini kujiendeleza katika
biashara zao,na kurudisha mikopo hiyo kwa njia ya M-PESA.
Mwenyekiti wa kikundi cha tupendane
Bi.Rosena Rashid -Mkazi wa Tarafa ya Matombo Morogoro vijijini akisaini kitabu
cha orodha ya wakina mama wajasiriamali wadogowadogo waliokuwa wakipatiwa
mikopo ya pesa isiyokuwa na riba ya
zaidi ya shilingi Milioni 327 toka Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa
“MWEI”unaowawezesha wanawake wajasiriamali wadogowadogo nchini, na kurudisha
mikopo hiyo kwa njia ya M-PESA.anaeshuhudia kushoto ni Meneja Mawasiliano wa
Vodacom Tanzania Bi.Rukia Mtingwa.
Mwenyekiti wa kikundi cha tupendane
Bi.Rosena Rashid- Mkazi wa Tarafa ya Matombo Morogoro vijijini akipokea mkopo
wa pesa kutoka kwa wakala wa M-PESA wa Vodacom Morogoro,Bw.Verus
Bitahilo(alieketi)Kampuni hiyo inatoa mikopo kwa wanawake wadogowadogo
wajasiriamali hapa nchini isiokuwa na riba wanawake hao walipokea mkopo huo yenye
thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 327 kupitia mradi wake wa “MWEI” na kurudisha mikopo hiyo
kwa njia ya M-PESA.anaeshuhudia wapili toka kulia walioketi ni Meneja wa mradi
huo Bi.Grace Lyon.
Wakala wa M-PESA wa Vodacom Mkoani Morogoro,Bw.Verus
Bitahilo(alieketi)akimkabidhi Mwenyekiti wa kikundi cha Mother support
Bi.Veronica Nyemele- Mkazi wa Tarafa ya Matombo Morogoro vijijini Mkazi wa,mkopo
wa kiasi cha shilingi 100,000 usiokuwa na riba unaotolewa na Vodacom kupitia
mradi wake wa “MWEI”unaowawezesha
wanawake wajasiriamali wadogowadogo nchini,waliopatiwa mkopo wa zaidi ya
shilingi Milioni 327 wilayani hapo.
Mwenyekiti wa kikundi cha Mother support
Bi.Veronica Nyemele- Mkazi wa Tarafa ya Matombo Morogoro vijijini akionesha na kufurahia pesa zake alizopewa mkopo usio na riba
toka Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa “MWEI”unaowawezesha wanawake wajasiriamali wadogowadogo
nchini, wanawake 7500 walinufaika na mkopo huo wa zaidi ya shilingi Milioni
327.
Kikundi cha Mother support wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kupatiwa mikopo hiyo.
Kikundi cha Mother support wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kupatiwa mikopo hiyo.
No comments:
Post a Comment