Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk
Emmanuel Nchimbi akitoa hotuba yake kwa wahitimu wa mafunzo ya Awali ya Polisi
na Uhamiaji (hawapo pichani) kabla ya kuyafunga mafunzo hayo katika Uwanja wa
Chuo Cha Polisi (CCP) mjini Moshi. Wahitimu 3,092 wakiwemo askari wa Uhamiaji 51
walimaliza mafunzo hayo juzi. Dk. Nchimbi katika hotuba yake aliwataka wahitimu
hao kufanya kazi kwa uadilifu katika vituo mbalimbali vya kazi watakavyopangiwa
nchini. (Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akikagua
guard ya wahitimu wa Jeshi la Polisi na Uhamiaji kabla ya kuyafunga mafunzo ya
wahitimu hao ya awali yaliyofanyika katika Chuo Cha Polisi (CCP) mjini Moshi
juzi. Wahitimu 3,092 wakiwemo askari wa Uhamiaji 51 walimaliza mafunzo hayo.
Dk. Nchimbi katika hotuba yake aliwataka wahitimu hao kufanya kazi kwa uadilifu
katika vituo mbalimbali vya kazi watakavyopangiwa nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi
(kulia) akimkabidhi zawadi mmoja wa wahitimu waliofanya vizuri katika masomo
yao wakati wa mafunzo ya awali ya Polisi na Uhamiaji yaliyofanyika katika Chuo
Cha Polisi (CCP) mjini Moshi juzi. Wahitimu 3,092 wakiwemo askari wa Uhamiaji
51 walimaliza mafunzo hayo leo. Dk. Nchimbi katika hotuba yake aliwataka
wahitimu hao kufanya kazi kwa uadilifu katika vituo mbalimbali vya kazi
watakavyopangiwa nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi
akifungua bomba la maji la kisima baada ya kukizindua katika Chuo Cha Polisi
(CCP) mjini Moshi juzi. Dk Nchimbi pia alitembelea miradi mbalimbali iliyopo
ndani ya chuo hicho kabla ya kufunga mafunzo ya awali ya Polisi na Uhamiaji
namba 1/2012/2013.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi
(kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil pamoja
na viongozi mbalimbali wa wizara na maofisa wa Jeshi la Polisi wakati alipokuwa
anawasili katika viwanja vya Chuo Cha Polisi (CCP), mjini Moshi kwa ajili ya
kufunga mafunzo ya awali ya Polisi na Uhamiaji juzi.
No comments:
Post a Comment