TANGAZO


Monday, July 15, 2013

Shehena ya kwanza ya mabomba ya kusafirishia gesi kutoka Mtwara na Songosongo kwenda Dar es Salaam yapakuliwa bandarini, Waziri Mkuu Pinda azindua upakuzi wake, anena, gesi kuwanufaisha wazawa

Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Balozi Lu Youging  akizungumza jambo na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), wakati wa uzinduzi wa upakuaji wa shehena ya kwanza ya mabomba ya kusafirishia gesi kutoka Songosongo na Mtwara kuja Dar es Salaam, bandarini Dar es Salaam juzi, ambapo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alizindua upakuzi huo. (Picha zote na Frank Shija  - MAELEZO)
Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Jambo Freight Forwarder, Vanessa Gwau (kushoto) akielezea jambo kwa mwandishi wa habari wakati wa hafla ya kupokea mabomba yatakayotumika kusafirisha gesi kutoka Mtwara na Songosongo kuja Dar es Salaam. Jambo Freight ndiyo Kampuni iliyopewa zabuni ya kupakua shehena hiyo.
Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Jambo Freight Forwarder, Vanessa Gwau (kushoto) akielezea jambo kwa mwandishi wa habari wakati wa hafla ya kupokea mabomba yatakayotumika kusafirisha gesi kutoka Mtwara na Songosongo kuja Dar es Salaam. 
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China, Balozi Lu Youging (katikati) akimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, wakati wa hafla hiyo. Kulia  ni Wang Fang kutoka Ubalozi wa China. 
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini, Lu Youqing (katikati), akizungumza jambo na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki, wakati wa hafla hiyo juzi. Kulia  ni Wang Fang kutota Ubalozi wa China.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwasili katika eneo la Bandari ya Dar es Salaam juzi, tayari kwa kuzindua rasmi upokeaji wa shehena ya mabomba yatakayotumika katika ujenzi wa mradi wa kusafirisha Gesi kutoka Mtwara na Saongosongo hadi Dar es Salaam.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (katika), akibadishana mawazo na Waziri wa Nishati na Madini Profes a Sospeter Muhongo (kushoto). Kulia ni Balozi wa China nchini Tanzania,  Lu Youqing wakati wa hafla ya uzinduzi wa kupokea shehena ya kwanza ya mabomba kwa ajili ya mradi wa kusafirisha Gesi kutoka Mtwara na Songosongo hadi Dar es Salaam.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akishuhudia Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China, Lu Youqing alipokuwa akimalizia kufunua kitamba kama ishara ya uzinduzi rasmi wa upokeaji wa mabomba ya Gesi.
Wafanyakazi wa Bandari wakiwa katika zoezi la kupakua mabomba kutoka katika meli na kupakia kwenye Lori tayari kwa safari ya Mtwara na Songosongo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza mara baada ya kuzindua rasmi upokeaji wa mabomba ya gesi tayari kwa kusafishwa hadi Mtwara na Songosongo. 



Na Frank Shija - Maelezo

SERIKALI imewatoa hofu wananchi wa Mtwara kuhusu kunufaika kwao na gesi asilia iliyopatikana katika maeneo yao.

Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda alipokuwa akizindua rasmi upokeaji wa shehena ya mabonba ya gezi kwa ajili ya mradi wa bomba la kusafirishia Gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam mwisho ni wiki jijini Dare se Salaam.

Pinda amesema kuwa wananchi wa watanzania watanufainaka na mradi huo hasa hasa wakazi wa Mtwara kwakuwa vijana wengi watapata ajira wakati na baada ya kukamilika kwa ujenzi wa bomba hilo kwakuwa viwanda mbalimbali vitajengwa mkoani Mtwara kikiwemo kiwanda cha Saruji ambacho ujenzi wake umekwisha anza.

“Ndugu zangu wana Mtwara ni waambe tu wakati wa kunufaina na rasilimali ya Gesi sasa umefika,niseme tu mradi huu utakapokamilika fursa mbalimbali zitafunguka ikiwemo ajira kwa wakazi wa Mtwara”. Alisema Pinda. 

Kwa upande wake Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Chini hapa nchini Balozi Lu Youging amesema kuwa Tanzania itanufaika na mradi huu na kukua kiuchumi kwakuwa itapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi katika nishati na badala yake itazalisha nishati yakutosha.

Balozi huyo aliongeza kuwa kutpitia mradi huu Tanzania itaondokana na kuwa tegemezi katika shughuli zake za maendeleo kwa kuwa kuna hazina ya kutosha ya gesi asilia na itawanufaisha watanzania wenyewe na si vinginevyo.

Jumla ya mabomba 3400 yamepokelewa katika awamu ya kwanza ambapo awamu ya pili itapokelewa shehena yenye mabonmba 4600 katika bandari ya Mtwara.Inakadiriwa kuwa jumla ya shehena 12 zitatumika mpaka mradi utakapokuwa umekamilika.

No comments:

Post a Comment