TANGAZO


Monday, July 15, 2013

Vijana nchini Tanzania watakiwa kubadili fikra zao ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili

Mmoja wa Wakurugenzi wa Chimbo Scool of Thought aliyefahamika kwa jina moja  la Erick akielezea juu ya umuhimu wa kujisomea vitabu ili kukuza ufahamu na kuongeza maarifa kwa vijana, wakati wa kongamano la Vijana lililofanyika jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na  Frank Shija - Maelezo)
Baadhi ya washiriki wa kongamano la vijana kuhusu kuwa na fikra za kimkakati wakifuatilia mada kwa umakini mkubwa katika kongamano hilo, jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akiwasilisha mada kuhusu fikra za kimkakati kwa Vijana jana jijini Dar es Salaam katika Kongamano la vijana lililoandaliwa wa Kanisa la Nchi ya Ahadi kupitia kituo chake kinachojulikana kwa jina la CHIMBO School of Thought.
Mkurugenzi Mkuu wa Chimbo School of Thought Mchungaji Harris KapigA akielezea jambo katika Kongamano la vijana liloandaliwa na kituo hicho jana jijini Dar es Salaam.
Bwana Alexander Saba kijana aliyeshiriki kongamano hilo akifafanua jambo wakati wa kuchangia mada kuhusu vijana kuwa na fikra za kimkakati ili kujiletea maendeleo.
Baadhi ya washiriki wa kongamano la vijana kuhusu kuwa na fikra za kimkakati wakifuatilia mada kwa umakini mkubwa.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akiwasilisha mada kuhusu fikra za kimkakati kwa Vijana jana jijini Dar es Salaam katika Kongamano la vijana lililoandaliwa wa Kanisa la Nchi ya Ahadi kupitia kituo chake kinachojulikana kwa jina la CHIMBO School of Thought.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kongamano la vijana kuhusu fikra za kimkakati. 
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel aliyekaa katikati akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa CHIMBO School of Thought. 



Na Frank Shija Maelezo


VIJANA nchini, wametakiwa kuwa na fikra za kimkakati ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili katika kupambana na umasikini.
Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Tanzania kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel, alipokuwa akiwasilisha mada juu ya vijana kuwa na fikra za kimkakati katika kongamano lililoandaliwa na Kituo cha Vijana kinachojulika kwa jina la Chimbo School of Thought jijini Dar es Salaam.
Profesa Ole Gabriel amesema kuwa inakuwa ni tatizo kwa vijana kupambana na changamoto za maisha kwakuwa vijana wengi hawaweki mikakati katika fikra zao.
"Vijana mnapaswa kubadilika na kuanza kuwaza na kupanga mambo yenu kimkakati maana hakuna kitu kinafanikiwa bila ya kuwekewa mikakati,nah ii ndiyo maana mmekuwa mkikumbana na changamoto mbalambali na kukata tama," alisema Profesa Ole Gabriel.
Aidha, Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa takwimu zina onyesha takriban asilimia 35.1  ya idadi ya watu ni Vijana na ambapo vijana wanachua karibu asilimia 70 ya nguvu kazi,hivyo wasipo kuwa na fikra na kupanga mambo yao kimkakati nchi itapata hasara.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Chimbo School of Thought Mchungaji Harris Kapiga amesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa vijana kama nguvu kazi ya taifa kituo chake kimenuia kubadilisha vijana wengi nchini ili wawe na mitazamo chanya ili wajiletee maendeleo yao wenyewe.
Mchungaji Kapiga aliongeza kuwa kupitia kituo chake vijana wengi wamebadilika kimtazamo na kutoa wito kwa vijana wengi kushiriki katika makongamano mbalimbali yanayoandaliwa kwa ajili yao ili wajifunze na kupata ufahamu wa mambo mengi zaidi.

No comments:

Post a Comment