Bwana Harusi Damian akiwa amepozi na mke wake Skolastica katika sherehe za harusi yao iliyofanyika ukumbi wa Brigade Mess, jeshini Makongo Juu. |
Hapa wanaonesha shahada zao za ndoa |
Damian akitia saini kwenye shahada ya ndoa yake.
Skolastika akitia saini kwenye shahada ya ndoa iliyofungwa Kanisa la Katoliki la Makongo Juu jijini Dar es Salaam.
Ndugu jamaa na marafiki wakiwa kwenye ibaya ya sakramenti ya ndoa hiyo.
Hapa wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kanisa hilo baada ya kufunga ndoa.
Damian akionesha umahiri wa kumbeba mke wake baada ya kuachana na ukapera.
Hapa wakiwa na wazazi wao walezi Mzee Rugemalira na mke wake mama Rugemalira.
Wazazi wa maharusi hao wakiwa meza kuu, kutoka kushoto ni mke wa Boniface Katanyebile, Boniface, Mzee Rugemalira na mkewe Benedictor Rugemalira.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye sherehe hiyo.
Maharusi hao katikati wakiwa na wapambe wao. Kulia ni Avitus Mashone na mke wake Elizabeth Avitus.
Wasanii wa kundi la sanaa la Mabibo Beer, Wines and Spirits Ltd wakitoa burudani kwenye sherehe za ndoa hiyo zilizofanyika ukumbi wa Brigade Mess Jeshini Makongo Juu.
Wanachama wa Asasi isiyo ya kiserikali ya Makongo Hill Society wakiwa kwenye hafla hiyo.
Maharusi hao wakinyweshana mvinyo.
Wazazi walezi wa maharusi hao wakisubiri kupokea keki.
Hapa mama mlezi Benedictor Rugemalira akipokea keki kutoka kwa bibi harusi.
Wazazi wa bibi harusi wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mama Rugemalira akiwa na mjukuu wake aliyenyoa staili ya kipekee hakika mjukuu amependeza.
Mzee James Rugemalira akiongoza vijana kusakata sebene.
Benedictor Rugemalira akitoa neno la kuwafunda maharusi hao.
Mshauri Biashara wa Kujitegemea wa Kimataifa wa Kampuni ya Mabibo Beer, Wines and Sipirits Ltd, James Rugemalira (kushoto), akizungumza na wadau mbalimbali Dar es Salaam jana katika harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Bugando jijini Mwanza. Harambee hiyo ilifadhiliwa na kampuni ya Mabibo ambapo zaidi ya sh. milioni 4 zilipatikana. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Benedictor Rugemalira.
Mzee Rugemalira akiwa na furaha baada ya vijana wake hao kufunga ndoa.
Bwana harusi akikabidhiwa zana za kimila mkuki na mundu kwa ajili ya kujilinda.
Mama mlezi Benedictor Rugemalira akimfunga mkoja bibi harusi.
Maharusi hao wakikabidhiwa biblia iwe silaha katika maisha yao.
Hapa wazazi wa bibi harusi wakienda kuwatuza maharusi hao zawadi mbalimbali.
Hapa wageni waalikwa wakiserebuka baada ya kupata msosi wa nguvu na vinywaji mbalimbali kutoka Kampuni ya Mabibo Beer, Wines and Spirits Ltd. Ni kwaito na bolingo kwa kwenda mbele.
No comments:
Post a Comment