TANGAZO


Friday, July 26, 2013

Wananchi wa Mji wa Babati mkoani Manyara watoa maoni kuhusu Rasimu ya Katiba


1.
Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmshauri ya Mji wa Babati Mjini Mkoani Manyara, Bw. JanesDabare (kulia) akichangia hoja katika eneo la mihimili ya Dola katika Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji huo leo Ijumaa, Julai 26, 2013.
2.
Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara wakiwa katika mjadala wa kuipitia Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji huo leo Ijumaa, Julai 26, 2013.
3.
Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmshauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara, Bi. Catherine Lucas (kushoto), Kasturi Silveri (katikati) na Hiiti Nyabasi wakipitia  vifungu vilivyopo katika Rasimu ya Katiba Mpya katika mkutano wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji huo leo Ijumaa, Julai 26, 2013.
4.
Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmshauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara, Bw. AskariEmeda (kushoto) na Bi ZubedaIddi wakisoma vipengele vilivyopo katika Rasimu ya Katiba Mpyailiyotolewa naTume ya Mabadiliko ya Katiba wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji huo leo Ijumaa Julai 26, 2013.
5.
Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara, Bw. Askari Emeda akichangia hoja wakati wa mkutano wa kuijadili Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji huo leo, Ijumaa Julai 26, 2013.
6.
Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara Bw. Simon Mahenge akichangia hoja wakati wa mkutano wa kuijadili Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa naTume ya Mabadiliko ya Katiba uliofanyika leo, Ijumaa Julai 26, 2013. (Picha zote na Tume ya  Katiba)

No comments:

Post a Comment