TANGAZO


Friday, July 26, 2013

Maandamano yafanyika nchini Tunisia




Mohamed Brahmi
Tunisia inashuhudia mgomo wa taifa zima baada ya kuuawa kwa kiongozi wa upinzani Mohamed Brahmi.
Chama cha wafanyakazi kikubwa kuliko vyote nchini Tunisia, UGTT, kimetoa wito wa kuwataka wananchi kupinga "ugaidi, ghasia na mauaji".
Alhamisi polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji katika miji kadhaa nchini humo, baada ya Bwana Brahmi kuuawa kwa kupigwa risasi nje ya nyumba yake mjini Tunis.
Chama tawala nchini Tunisia, cha Kiislam cha Ennahda kimekanusha tuhuma kutoka kwa ndugu wa marehemu kuwa kilikula njama katika mauaji ya Bwana Brahmi.

No comments:

Post a Comment