Naibu Mkurugenzi wa Mipango, Uchaguzi na Siasa wa Chama cha Wananchi (CUF), Shaweji Mketo, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu maandamano ya amani yatakayofanywa na chama hicho, kuelekea Ikulu Juni 29, mwaka huu. Kushoto ni Ofisa Utawala na Uendeshaji wa CUF, Twaha Rashid.
Naibu Mkurugenzi wa Mipango, Uchaguzi na Siasa wa Chama cha Wananchi (CUF), Shaweji Mketo, akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari, wakati alipozungumza nao, jijini Dar es Salaam leo, kuhusu maandamano ya amani yatakayofanywa na chama hicho kuelekea Ikulu Juni 29, mwaka huu. Kushoto ni Ofisa Utawala na Uendeshaji wa CUF, Twaha Rashid. Naibu Mkurugenzi wa Mipango, Uchaguzi na Siasa wa Chama cha Wananchi (CUF), Shaweji Mketo, akifafanunua jambo kwa waandishi wa habari, wakati alipokuwa akizungumza nao, kuhusu maandamano ya ya amani yatakayofanywa na chama hicho, kuelekea Ikulu kumuona Rais Jakaya Kikwete kuhusiana na kunyanyaswa kwa watu wa Wamtwara, kuporwa vitu na Polisi pamoja na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), majumbani mwao. Maandamano hayo, yatafanyika Juni 29, mwaka huu. Kushoto ni Ofisa Utawala na Uendeshaji wa CUF, Twaha Rashid.
Na Hamisi Magendela
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba anatarajiwa kuongoza maandamano ya amani, Juni 29 mwaka huu kwenda Ikulu kwa ajili ya kuonana na Rais Jakaya.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Naibu Mkurugenzi wa Mipango, Uchaguzi na Siasa, Shaweji Mketo alisema lengo la kufanya maandano hayo ni kufikisha malalamiko ya wananchi kutokana na vitendo vya ukatili anavyodai kufanywa na Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi (JWTZ) dhidi ya wananchi.
Aliongeza kuwa Juni 15 mwaka huu wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikihitimisha kampeni zake za uchaguzi mdogo wa udiwani, katika Kata nne mkoani Arusha palitokea mlipuko wa bomu uliopoteza maisha ya watu wanne, hivyo jambo hilo si la kwanza kutokea katika mikutano ya kisiasa na kuundwa Tume.
"Chama cha CUF hakikusudii kuingilia uchunguzi unaoendelea lakini tunataka kufikisha ujumbe kwa rais kwamba hii si mara ya kwanza kuundwa kwa tume ya uchunguzi kwa tukio kama hilo lakini kinachotusikitisha, hata baada ya majibu ya yanapokamilika kuhusu uchunguzi kunakuwa hakuna taarifa yoyote inayotangazwa hadharani pamoja na wahusika kutochuliwa hatua za kisheria," alisema.
Alifafanua kuwa maandamano hayo yataanza saa nne asubuhi katika eneo la Buguruni kituo cha Mafuta, kupitia barabara ya Uhuru, Mnazi mmoja, Bibi Titi, Posta mpya , Ardhi hadi Ikulu.
Aliongeza kuwa chama hicho kilianzishwa kwa madhumuni ya kuwaunganisha watanzania wote popote walipo, bila kujali itikadi zao na waweze kukataa aina yoyote ya uonevu, ukandamizaji, unyanyasaji, ubaguzi na udhalilishaji wa kisiasa au kiuchumi.
Pia alisema wanadhamira ya kulinda, kutekeleza na kuenzi haki za binadamu pamoja na kuinua uchumi wa nchi kwa siasa zitumikie uchumi badala ya uchumi kutumikia siasa kama inavyofanyika hivi sasa.
Aliongeza kuwa maisha ya manyanyaso kwa raia hayawezi kuendeshwa katika nchi huru kama Tanzania badala yake mambo hayo yanakumbusha enzi za utawala wa kikoloni ambapo Cuf kamwe haipo tayari kuruhusu vitendo vya haina hiyo kuona vikiendelea kufanyika nchini.
"Tunaamini siasa za ustaharabu zitawezesha kuwa na jamii salama yenye mshikamano na ushirikiano katika kuijenga nchi yetu, lakini wenzetu wanatumia upole wetu na ustaharabu wetu kutufanyia vitendo vinavyokiuka utu wa mtu na hatimaye kila aliyepewa mamlaka ya kuongoza sehemu ya nchi yetu anageuka kuwa mfalme na kuamrisha kamata yule, mpe kesi yule na mwache yule, alisema.
Alifafanua kuwa taifa la Tanzania litajengwa na watanzania wenyewe kwa kushirikiana na kusikilizana, amani ya kweli itapatikana ikiwa haki itaonekana kutendeka kwa jamii yote na hayo yatakuwa ni sehemu mambo watakayoyawasilisha kwa Rais ili ayafanyie kazi.
Pia alisema kuwa ujio wa Rais wa marekani hautaathiri maandano yao kwani watafanya hivyo kwa lengio la kudumisha amani ya nchi na si vinginevyo na wanaamini kusudio hilo litafanikiwa bila kuwepo pingamizi lolote.
No comments:
Post a Comment