TANGAZO


Saturday, June 22, 2013

Jeshi la Magereza nchini laazimisha Siku ya Magereza Kitaifa



Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Abdull Wakili (katikati), akikagua gwaride katika maadhimisho ya siku ya Magereza zilizofanyika Dar es Salaam leo katika viwanja vya Chuo cha maofisa wa Jeshi la Magereza Ukonga Dar es Salaam.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Abdull Wakili (kushoto),  na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini John Minja na Kamishna wa Utawala na Fedha, Gaiton Sanga, wakipata maelekezo kutoka kwa Mrakibu  Mwandamizi wa Jeshi la Magereza , Janeth Keha (wa pili kulia), kuhusu vitabu vya sheria vya jeshi hilo.
 Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP), Alexander Mmasi (kushoto), akimuonesha mgeni rasmi wa hafla hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Abdull Wakili  (kulia), samani mbalimbali zinazotengenezwa na jeshi hilo katika 
maonesho ya bidhaa mbalimbali ikiwa ni sehemu ya sherehe hizo. Katikati ni Kamishna wa Magereza Dionice Chamlesile.
Wananchi na familia za askari Magereza wakifuatilia mambo mbalimbali kwenye sherehe hizo.
Askari pekee wa kike wa jeshi hilo aliyeko mafunzoni katika kikosi maalumu cha KMKM (kushoto), akionesha jinsi ya kupambana na adui mbele ya mgeni rasmi.
Askari wa Kikosi Maalumu cha jeshi hilo maarufu kama KMKM wakitoa heshima  mbele ya mgeni rasmi baada ya kuonesha michezo mbalimbali inayoonesha jinsi ya kukabiliana na adui. 
Maofisa wa Magereza wakiwa kwenye hafla hiyo.
Watoto wa familia za askari Magereza wakifuatilia mambo mbalimbali kwenye sherehe hizo.
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini John Minja (kulia), akutoa hutuba fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi wa sherehe hizo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo, Abdull Wakili. Kushoto ni Kamishna wa Utawala na Fedha, Gaiton Sanga.
Maofisa wa jeshi la Magereza na wageni waalikwa wakiwa kwenye sherehe hizo.
 Mkaguzi wa Magereza, Tumaini Kihampa, akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea Kitengo cha kupokea taarifa za wafungwa na mahabusu wanapoingia na kutoka katika magereza baada ya kumaliza vifungo vyao na kupewa dhamana.
Maofisa wa Magereza wakifuatilia matukio mbalimbali ya sherehe hizo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Abdull Wakili
(kulia), akihutubia kwenye maadhimisho hayo. Kushoto ni Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi hilo, Gaiton Sanga na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini John Minja.(Picha zote na Dotto Mwaibale)

No comments:

Post a Comment