Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni simu Tanzania (TTCL), Said Amir Said. akifafanua jambo wakati wa semina ya Mkongo wa Mawasiliano iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam na kuwashirikisha wahariri wa vyombo mbalimba vya habari. Kushoto ni Meneja Uendeshaji wa kampuni hiyo, Adin Mgendi.
DAR ES SALAAM, Tanzania
SERIKALI imesema kuwa mradi wa mkongo wa Taifa wa mawasiliano ukisimamiwa
na kuendeshwa kwa uaminifu utachangia maendeleo ya nchi ikiwemo kulipa mkopo
uliotumika kuujenga.
Mradi huo ambao utapanua soko la mawasiliano kutoka nchi moja
hadi tisa.
Akizungumza ijini Dar es Salaam leo wakati wa kufungua semina
ya wahariri wa vyombo vya habari Mkurugenzi wa Tehama, Injinia Zaipuna Yonah,
alisema kuwa manufaa ya mkongo huo wa mawasiliano yameshaanza kuonekana hasa
baada ya kuongezeka ubora na kasi ya matumizi ya mtandao na data pamoja na
utoaji wa huduma za elimu mtandao.
Yonah alisema kuwa faida za mkongo zinaonekana na zimekidhi
matarajio ya Serikali ya kuziba pengo la matumizi ya Tehama kwa wananchi na
kukuza uchumi.
Akizitaja changamoto zilizojitokeza alisema kuwa ni usalama wa
miundo mbinu ambayo inapita kwenye makazi ya watu, mashambani, hifadhi za
wanyama na kuwataka watanzania kuhakikisha rasilimali niyo inatunzwa.
Pia alisema kuwa Serikali imeikabidhi kampuni ya simu (TTCL)
kuhakikisha inasimamia, inaendesha na kuuendeleza mkongo wa mawasiliano ili
kuleta mabadiliko ya utendaji na ufanisi wa kazi kupitia Serikali mtandao,
elimu mtandao, afya mtandao, kilimo mtandao na kujenga utamaduni mpya wa
wanachi kupata taarifaza serikali kwa uwazi.
No comments:
Post a Comment