Pichani ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Rungwe Mpya na Asante Nyerere katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Rungwe Mpya, Kata ya Rungwe Mpya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi
(CCM), Nape Nauye ametembelea Kijiji cha Rungwe Mpya kilichopo kata ya Rungwe Mpya Wilayani
Kasulu, mkoani Kigoma na kufanya shughuli mbalimbali za Chama ikiwa ni pamoja na
Kuweka jiwe la Msingila la Ofisi ya CCM kijijini hapo na kuhutubia mkutano wa
hadhara wa wananchi wa Kata hiyo.
Baada ya kuweka Jiwe hilo la Msingi, Nnauye
alikabidhi kadi kwa wanachama wapya wa Chama hicho kutoka katika kata za Asante
Nyerere pamoja na Rugwe Mpya, wanachama ambao wamerejea CCM kutoka vyama vya
upinzani hasa NCCR Mageuzi na Chadema.
Aidha Nape pia alipata fursa ya kuzungumza na
Wajumbe wa Nyumba Kumi wa chama hicho, Wazee pamoja na Vijana waendesha Bodaboda
mjini Kasulu.
Nape akikabidhi kadi kwa wanachama
wapya wakati wa mkutano0 huo.
Baadhi ya Kadi zilizorejeshwa.
Mkuu wa Wilaya Kasulu, Danny Makanga akicheza
ngoma wakati wa mapokezi hayo, ya Nape Kijijini hapo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape
Nnauye akiweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Ofisi ya CCM Kijijini hapo.
No comments:
Post a Comment