Mchezaji Frank Senkule wa Simba akiwatoka Sunday Frank (nyuma) na Sahim Nuhu wa Azam FC, wakati wa mchezo wa nusu fainal ya michuano ya BancABC, Sup8r 2012 kati ya timu hizo, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.
Ibrahim Hayib wa Simba (kuia), akimpiaga chenga Ibrahim Chimwanga wa Azam FC katika mchezo huo leo jioni.
Edward Christopher wa Simba (kulia), akimtoka Ibrahim Chimwanga wa Azam FC katika mchezo huo.
Mchezaji Sahim Nuhu wa Azam FC, akiutoa mpira miguuni mwa Frank Senkule wa Simba wakati wa mchezo huo wa nusu fainal ya michuano ya BancABC, Sup8r 2012, uliofanyika leo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mashabiki wa Simba wakiishangilia timu yao baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Taifa jijini leo.
Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo kati ya timu yao na Azam FC, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.
Ramadhan Mzee wa Simba, akiwatoka Said Morad na Abdulhalim Humud (kushoto) katika mchezo huo wa nusu faina ya michuano ya BancABC Sup8r 2012, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Ramadhan Mzee wa Simba, akiuzuiya mpira kwa ajili ya kujaribu kuwapiga chenga Said Morad na Abdulhalim Humud (kushoto) katika mchezo huo wa nusu faina ya michuano ya BancABC Sup8r 2012, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Wachezaji wa Simba wakishangilia ushindi huo huku wakiwa wamembeba kocha wao, Suleiman Matola mara baada ya kumalizika mchezo baina ya timu hizo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya timu ya Simba, Hans Pop (kushoto), akimkabidhi jezi namba 5, beki wao mpya kutoka Kenya Pascal Ocieng katika mkutano huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya timu ya Simba, Hans Pop (kushoto), akimkabidhi jezi namba 13, mshambuliaji wao mpya kutoka Ivory Coast, Damiane Okufor katika mkutano huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.
Wachezaji wapya wa Simba, Pascal Ocieng (kulia) na Damiane Okufor wakiwa katika mkutano wa utambulisho kwa waandishi wa habari, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.
No comments:
Post a Comment