NMB KARIBU YAKO WAKATI WA RAMADHAN
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki ya NMB, Imani Kajula (kushoto), akimkaribisha Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga katika futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo, mjini Zanzibar jana. Anayeshuhudia ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Salie Mlay.
Kamishna wa Polisi Zanzibar, Musa Ali Musa (wa pili kulia), akisalimiana na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NMB, Imani Kajula wakati wa futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wa NMB Zanzibar. Katikati ni Meneja wa NMB Zanzibar, Mluku Maggid.
Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga (kulia), akipeana mkono na Ofisa wa Huduma kwa Wateja wa benki ya NMB Zanzibar, Haji Dau wakati wa futari ya wateja wa NMB wa mjini Zanzibar jana. Katikati ni Meneja wa NMB Zanzibar, Mluku Maggid.
Meneja wa NMB Zanzibar, Mluku Maggid akizungumza na wateja wa NMB waliofika katika futari iliyoandaliwa kwa ajili yao na benki hiyo.
Meneja wa benki ya NMB Zanzibar, Mluku Maggid (kushoto), akizungumza na mmoja wa maofisa wa NMB Zanzibar. Katikati ni Meneja Masoko wa NMB, Shilla Senkoro.
Wateja wa benki ya NMB Zanzibar, wakiwa kwenye picha ya pamoja na maofisa wa NMB mara baada ya futari waliyoandaliwa na benki hiyo. (Picha zote na mdau wetu)
No comments:
Post a Comment