TANGAZO


Wednesday, August 15, 2012

Rais Shein awaandalia futari wananchi wa Tunguu kisiwani Unguja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kulia), akijumuika na wananchi pamoja na viongozi wa Mkoa wa Kusini Unguja katika futari, aliyowaandalia wananchi hao, huko viwanja vya jengo la Ofisi ya Uhamiaji Tunguu, Wilaya ya Kati Unguja jana. 

Baadhi ya wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Kusini Unguja, wakiwa katika  chakula cha futari, iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein katika viwanja vya jengo la Ofisi ya Uhamiaji, Wilaya ya Kati Unguja jana.

Baadhi ya akina mama wa kijiji cha Mkanyageni, Mkoa wa Kusini Unguja, wakiwa katika  chakula cha futari, iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein katika viwanja vya jengo la Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Kati Unguja jana.

Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mwanamwema Shein (katikati), akijumuika na akinamama wa Mkoa wa Kusini Unguja katika chakula cha futari, iliyoandaliwa kwa wananchi hao na Rais wa Zanzibar, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein katika viwanja vya jengo la Ofisi ya Uhamiaji, Wilaya ya Kati Unguja jana.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, akiitikia dua na viongozi pamoja na wananchi wa Mkoa wa Kusini, Unguja jana, iliyoombwa na Mufti wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kabi, baada ya chakula cha futari, iliyofanyika katika viwanja vya jengo la Ofisi ya Uhamiaji, Tunguu Wilaya ya Kati Unguja jana.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto), akisalimiana na viongozi na wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja, mara  baada ya kufutari nao pamoja jana katika futari aliyowaandalia huko viwanja vya jengo la Ofisi ya Uhamiaji Tunguu, Wilaya ya Kati. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)

No comments:

Post a Comment