Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa akiingia kwenye ukumbi wa Bunge leo, tayari kwa maandalizi ya kusoma hotuba ya Wizara yake ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013, mjini Dodoma.
Baadhi ya Masheikh 69 wa Jimbo la Iramba Magharibi wakiwa na Mbunge wao, Mwigulu Mchemba (katikati aliyevaa skafu), wakati walipofika Bungeni leo kwa mwaliko wake, kuangalia shughuli mbalimbali za Bunge, mjini Dodoma leo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (katikati), aliyevaa suti nyeusi, akiwa na baadhi ya Masheikh 69 wa Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza nao kuhusu sensa, akisisitiza juu ya kuwaelimisha waumini wao juu ya umuhimu wa sensa kwa maendeleo ya Taifa. Masheikh hao ambao walikuwepo Bungeni leo kwa mwaliko wa Mbunge wao, Mwigulu Mchemba.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (katikati), aliyevaa suti nyeusi, akiwa na baadhi ya Masheikh 69 wa Jimbo la Iramba Magharibi akipiga nao picha ambapo pia alizungumza nao kuhusu umuhimu wa sensa, akisisitiza juu ya kuwaelimisha waumini wao juu ya umuhimu wa sensa kwa maendeleo ya Taifa. Masheikh hao ambao walikuwepo Bungeni leo kwa mwaliko wa Mbunge wao, Mwigulu Mchemba.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (katikati), aliyevaa suti nyeusi, akiwa na baadhi ya Masheikh 69 wa Jimbo la Iramba Magharibi akipiga nao picha ambapo pia alizungumza nao kuhusu umuhimu wa sensa, akisisitiza juu ya kuwaelimisha waumini wao juu ya umuhimu wa sensa kwa maendeleo ya Taifa. Masheikh hao ambao walikuwepo Bungeni leo kwa mwaliko wa Mbunge wao, Mwigulu Mchemba. (Picha zote na mdau wetu)
No comments:
Post a Comment