TANGAZO


Friday, August 17, 2012

Shirika la Simu Tanzania (TTCL) latoa zawadi ya Idi kwa vituo vya yatima Dar es Salaam


 Ofisa Mtendeaji Mkuu wa Shirika la Simu Tanzania (TTCL), Said Amir Said, akikabidhi zawadi za Sikukuu ya Idi kwa Sista Mary Grisaldia na Mary Annie kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima cha Mama Teresa kilichopo Mburahati jijini Dar es Salaam leo.

 Watoto wa kituo cha kulelea yatima cha Msongola, Kivule Kitunda jijini Dar es Salaam, Maria Daniel na Neema James, wakipokea sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali vilivyotolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Simu Tanzania (TTCL), Said Amir Said  kwa ajili ya Sikukuu ya Idi. 
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Simu Tanzania (TTCL), Said Amir Said, akiwa katika picha ya pamoja na walezi wa vituo vilivyopewa misaada pamoja na baadhi ya yatima wa kituo hicho.

Baadhi ya walezi na Wakurugenzi wa vituo vya kulelea yatima jijini Dar es Salaam wakiwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari na wafanyakazi wa Shirika la Simu Tanzania, wakiwa katika hafla hiyo, jijini leo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Simu Tanzania (TTCL), Said Amir Said akifafanua jambo kabla ya kukabidhi msaada wa vyakula kwa vituo vya yatima jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment