TANGAZO


Friday, August 17, 2012

Rais Shein awaandalia futari viongozi na wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi

Baadhi ya wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, wakianza kufutari kwa  kunywa maji ya madafu kabla ya kula futari jana walipoalikwa katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, ikiwa ni kawaida yake kuwaalika wananchi wa Mkoa huo, kila ifikapo mwezi kama  huu kwa futari maalum. (Picha zote na Ramadhan
Othman, Ikulu)

Baadhi ya viongozi, wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, wakiwa katika  chakula cha Futari katika Mwezi mtukufu wa Ramadhan, iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar jana.

Baadhi ya akina mama wa Mkoa wa Mjini Magharibi, wakiwa katika  chakula cha Futari, kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Ikulu ya mjini Zanzibar jana.

Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mwanamwema Shein (wa pili kushoto), akijumuika na akina mama wa  Mkoa wa Mjini Magharibi katika  chakula cha Futari, kilichoandaliwa kwa wananchi hao na Rais wa Zanzibar, Alhaj Dk. Ali
Mohamed Shein, katika viwanja vya Ikulu, mjini Zanzibar jana. Wengine kulia ni Mama Shadiya Karume, Mama Pili Seif na Waziri wa Muungano na kushoto ni Samia Suluhu Hassan.

Baadhi ya wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, wakiwa katika futari iliyoandaliwa  jana ,katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanibar  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, ikiwa ni
kawaida yake kuwaalika wananchi wa Mkoa huo, kila ifikapo mwezi kama huu kwa futari maalum .

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kulia), akijumuika na wananchi pamoja na viongozi wa Mkoa wa Mjini Magharibi katika Futari, aliyowaandalia wananchi hao katika  viwanja vya Ikulu, mjini Zanzibar jana. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdalla Mwinyi Khamis, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Amaan Abeid Karume,(kushoto)  na Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi.

Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mwanamwema Shein (kulia), akisalimiana na mke wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Mama Shadya Karume, baada ya Futari iliyoandaliwa kwa wananchi wa Mkoa wa mjini Magharibi na Rais wa Zanzibar, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, viwanja vya  Ikulu, Mjini Zanzibar jana.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, na  Mkewe Mama Mwanamwema Shein, wakisalimiana na viongozi na wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, baada ya kumalizika kwa futari waliyowaandalia  katika viwanja vya Ikulu, mjini Zanzibar jana.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein,  akisalimiana na viongozi  na wananchi wa Mkoa wa  Mjini Magharibi, baada ya kufuturu nao pamoja jana katika futari aliyowaandalia   katika  viwanja vya Ikulu ya Mjini Zanzibar

No comments:

Post a Comment