TANGAZO


Friday, August 17, 2012

Mkutano wa Simba, Mtibwa katika kufikia mpambano wao wa Fainali ya BancABC Sup8r 2012

Mkurugenzi Mkuu wa Fedha wa BancABC, Mwalimu Zubery, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, kuhusu pambano la fainali la mashindao ya BancABC Sup8r 2012 kati ya Simba na Mtibwa FC, litakalochezwa leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Wa pili ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah, kocha wa Mtibwa, Mecky Maxime na Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah, akizungumza katika hafla hiyo. Katikati ni kocha wa Mtibwa, Mecky Maxime na Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga.

 Baadhi waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakiwa katika mkutano huo, Ofisi za BancABC, Quality Centre, Dar es Salaam leo.

 Mmoja wa viongozi wa timu ya Mtibwa, akizungumza katika mkutano huo.

Kocha wa Mtibwa, Mecky Maxime, akizungumza katika mkutano huo, kueleza maandalizi na matarajio ya timu yake katika mchezo wa kesho dhidi ya Simba. 

  Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, akizungumza katika mkutano huo, kuelezea matarajio ya kikosi chake katika kulinyakua kombe hilo la BancABC Sup8r 2012, kesho.

 Mmoja wa viongozi wa Kiwohede, akizungumza katika mkutano huo.

 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah, akizungumza katika hafla hiyo. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Fedha wa BancABC, Mwalimu Zubery.

Baadhi ya wachezaji wa timu ya Simba wakiwa kwenye mkutano huo.

No comments:

Post a Comment