Baraza kuu la Umoja wa mataifa limeidhinisha kura ya azimio kuhusu Syria sawa na ile iliyopigiwa kura ya turufu na Urusi na Uchina katika baraza la usalama la umoja huo.
Azimio hilo linalaani mashambulizi yanayotekelezwa na serikali ya Syria dhidi ya wapinzani wake.
Linaunga mkono mpango uliopendekezwa na juimuiya ya nchi ya kiarabu kuhusu mageuzi ya kisiasa nchini humo, ambapo Rais Bashar al Assad ataondoka mamlakani.
Azimio hilo halinatofauti sana na lile ya baraza la usalama la umoja huo ambalo lilipingwa na Urusi na china.
Na kama ilivyo tarajiwa nchi hizo mbili zilipiga kura kupinga azimio hilo.
Hata hivyo waliopendekeza azimio hilo sasa watajigamba kuwa wamepata kuungwa mkono na sehemu kubwa ya wanachama wa umoja wa mataifa.
Urusi ilipinga azimio hilo kuwa halijasisitiza kuwa pande zote mbili hasimu lazima zisitishe mashambulio na pia kuwa mazungumzo yoyote kuhusu mustakabal wa kisiasa wa Syria lazima yahusishe utawala wa sasa.
Baraza kuu la Umoja wa Mataifa halina nguvu za kisheria kushinikiza utekelezwaji wa azimio hilo kwa hivyo matokeo haya hayana uzito sana ila tu kuongeza shinikizo kwa serikali ya syria ikomeshe ghasia zinazo endelea.
No comments:
Post a Comment