Klitschko amesema atalipiza kisasi ulingoni kwa kuzabwa kofi na Chisora
Mwanandondi Muingereza ambaye ni mzaliwa wa Zimbabwe, Dereck Chisora amemzaba kofi mpinzani wake Vitali Klistchko kabla ya pambano lao la mjini Munich, Ujerumani, siku ya
Jumamosi.
Ripoti zasema Chisora alimrushia kofi Klitchko, ambaye ni bingwa mtetezi wa masumbwi ya uzani wa juu wa tawi la WBC, wakati wa kikao na waandishi wa habari baada ya wote wawili kupimwa uzani wao, tayari kwa pambano la mjini Munich, Ujerumani. Klitschko, ambaye ni raia wa Ukraine, alijizuia kujibu kofi hilo na kukitaja kitendo cha Chisora kama cha kustajabisha.
Chisora, mwenye umri wa miaka 28, amesema licha ya kukosa ujuzi, atampokonya Klitschko taji lake.
Kwa upande wake, Klitschko amejigamba kwamba hakuna upinzani wa kumbabaisha katika harakati za kutetea ubingwa wake.
No comments:
Post a Comment