TANGAZO


Friday, February 17, 2012

Washirika wa Gadafi kubuni vuguvugu

 
Aliyekuwa Rais wa Libya Muamar Gadaffi

Maafisa wakuu katika uliokuwa utawala wa Muamar Gadaffi, wanaoishi nje ya Libya, wananuia kuanzisha vuguvugu la kisiasa kuzuia kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Katika taarifa yao kwa BBC, mmoja wa viongozi hao, alielezea kuwa wanabuni vuguvugu litakaloitwa Libyan Popular National Movement.
Alisisitiza kutotambulishwa kwa kuhofia usalama wa familia yake nchini Libya.
Mwandishi wa BBC mashariki ya kati anasema utawala wa zamani nchini Libya ungali unaungwa mkono na baadhi ya raia wa nchi hiyo ingawa kubuni vuguvugu jipya itakuwa kibarua kikubwa, hasa baada ya kifo cha Gadafi huku mwanawe Seif al Islam, akiwa amekamatwa.

No comments:

Post a Comment