Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, atafanya mkutano wa maafisa wahusika, kuhusu ubaguzi katika kandanda.

Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron
Hayo yanafuatia visa kadha kama hivyo kwenye michezo.
 
Mkutano utajumuisha wawakilishi wa wachezaji na wakuu wa kandanda.
Tangazo hilo limekuja baada ya mchezaji mpira wa Uingereza, John Terry, kunyan'ganywa unahodha juma lilopita, kwa sababu ya shutuma kuwa alimtusi mchezaji mweusi.
Hatua ya Shirika la Kandanda la Uingereza kukataa John Terry kuwa nahodha wa timu ya Uingreza, ilipelekea meneja wa timu, Fabio Capello kujiuzulu, ambaye hajakubalina na uamuzi wa Shirika la Kandanda.