Jumuia ya nchi za Kiarabu imeamua kuuomba Umoja wa Mataifa uisaidie kuunda ujumbe wa amani wa pamoja, kuutuma Syria, ili kumaliza ghasia nchini humo.

Nabil El-Araby, Katibu Mkuu wa Jumuia ya Nchi za Kiarabu

Uamuzi huo ulifikiwa katika mkutano wa jumuia hiyo, unaofanywa Cairo.
Piya mawaziri walikubali kusitisha uhusiano wa kibalozi na Syria, na kuanza mazungumzo na upinzani wa Syria.
Mkuu wa Jumuia ya Nchi za Kiarabu, Nabil El-Araby, aliuambia mkutano kwamba wakati umefika kuchukua hatua thabiti kumaliza adhabu za watu wa Syria.