TANGAZO


Thursday, February 16, 2012

TIGO yasaidia kituo cha yatima cha New Life Orphans Home

 
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Simu ya tigo, Alice Maro, akila chakula cha mchana na watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika kituo cha kulelea watoto cha Life Orphans Home, Kigogo Dar es salaam leo Februari 16, 2012. (Picha na Richard Mwaikenda)

Msimamizi wa Masoko wa Kampuni ya simu ya tigo, Gaurdence Mushi (katikati), akila chakula cha mchana na watoto wa kituo hicho.


Baadhi ya Watoto wanaolelewa katika kituo cha New Life Orphans Home, wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya simu ya tigo wakati wa ziara ya wafanyakazi hao, kituoni hapo leo.

Watoto wakiwa na wafanyakazi wa Kampuni ya tigo, huku wakiwa washika mifuko yenye zawadi walizokabidhiwa na kampuni hiyo leo.


Wafanyakazi wa Kampuni ya Tigo wakichukua mifuko yenye zawadi kwa ajili ya kuwakabidhi watoto yatima wa kituo hicho.

Wasanii wakiburudisha kwa sarakasi wakati wa ziara ya wafanyakazi wa tigo kwenye kituo hicho.
Meneja wa Huduma za Burudani wa Kampuni ya tigo, David Zacharia (kushoto), akipokea risala kutoka kwa Kaka Mkuu wa kituo hicho, Issa Athumani.

Mkurugenzi wa Kituo hicho, Mwanaisha Magambo, akiwaonesha Maofisa wa Kampuni ya tigo, sehemu mbalimbali wanazoishi watoto wa kituo hicho.


Wafanyakazi wa Tigo, wakipatiwa maelezo na Mkurugenzi huyo.

No comments:

Post a Comment