Baadhi ya washiriki wa mkutano wa 16 wa Kimataifa wa Kamati ya Wataalamu (ICE), kuhusu Maendeleo ya Utawala wa Rasilimali Madini kwa nchi za Afrika, ulioandaliwa na Tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi kwa Afrika (UNECA), jijini Dar es Salaam, wakisikiliza mada juu ya umiliki wa ardhi kwa raia wa nchi za bara hilo.
Mshauri wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi kwa nchi za Kiafrika (UNECA), Profesa Lusuga Kironde, akielezea kuhusu mambo yanayoziathiri rasilimali za nchi za Kiafrika hadi kupelekea nchi hizo kutokunufaika nazo, wakati wa mkutano wa 16 wa Kimataifa wa Kamati ya Wataalamu (ICE), kuhusu Maendeleo ya Utawala wa rasilimali madini kwa nchi hizo, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mchumi Mwandamizi wa UN, Andrew Mold na Mkuu wa Malengo ya Sera (LPI) wa Umoja huo, Joan Kagwanja.
Mchumi Mwandamizi wa UN, Andrew Mold, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo, kuhusu kuanguka kwa uchumi wa Ulaya na kuimarika kwa uchumi wa nchi za Kiafrika wakati wa mtikisiko wa uchumi duniani. Kulia ni Mshauri wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi kwa nchi za Kiafrika (UNECA), Profesa Lusuga Kironde na katikati ni Mkuu wa Malengo ya Sera (LPI) wa Umoja huo, Joan Kagwanja.
Baadhi ya waandishi waliokuwa wakifuatilia mkutano huo, wakinukuu maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na wataalamu hao kwenye mkutano huo.
No comments:
Post a Comment