Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya
Bia Tanzania, Steve Kilindo (wa pili kushoto) na Meneja wa kinywaji cha Redd's, Victoria
Kimaro (kushoto), wakigongesha chupa za kinywaji hicho na baadhi ya warembo waliokwisha kushiriki mashindano ya urembo, wakati wa uzinduzi wa
udhamini wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania, ambayo sasa yatajulikana kama Redd's Miss Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika usiku wa kuamkia leo, ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam. (Picha na Richard Mwaikenda)
Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa TBL, Steve Kilindo (kushoto) na warembo wakiwa katika picha ya pamoja huku wakiwa wameshikilia chupa za kinywaji cha Redd's katika hafla hiyo.
Mtangazaji Dida wa Mchopsi (kushoto) wa Clouds, akiwa pamoja na marafiki zake katika hafla hiyo.
Furaha Samalu wa DSTV (kushoto), akiwa pamoja na Maofisa wa Kampuni ya Simu ya Zantel, wakifurahia jambo wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Awaich Mawalla ambaye ni Mkuu wa Bidhaa na Mawasiliano wa kampuni hiyo.
Miss Tanzania 2011, Salha Israel (katikati), akiwa na baadhi ya viongozi wa Kampuni ya Lino Iternational Agency, inayoaandaa mashindano hayo.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa TBL, Steve Kilindo, akizungumza wakati wa uzinduzi wa udhamini huo.
Mshereheshaji, Taji Liundi, akiwa kazini katika hafla ya uzinduzi huo.
Baadhi ya waandishi wa habari waliokuwepo katika hafla hiyo, wakifurahia jambo. Kutoka kulia ni Seleman Mbuguni wa Majira, Somoe Ng'itu wa Nipashe na Khadija Kalili wa Tanzania Daima.
Mkurugenzi wa Kianda cha Konyagi Tanzania, David Mgwassa (wa pili kulia) akiwa na baadhi ya viongozi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Kushoto ni Steven Kilindo.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Konyagi Tanzania, David Mgwassa (kushoto), akizungumza na kiongozi mwenzake wa kiwanda hicho, katika hafla hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa, wakijipatia vinywaji katika hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment