Macky Sall na Rais Wade katika mchuano mkali wa Urais

Rais wa Senegal Abdoulaye Wade amekiri kutopata kura za kutosha kuzuia duru ya pili uchaguzi isifanyike tena.
Hata hviyo ameelezea matumaini ya kunyakua tena uongozi wa nchi.
Matokeo yasiyo rasmi yameonyesha Bw Wade amepata 32% akiwa mbele ya mpinzani wake wa karibu, Macky Sall aliyepata 25% ya kura.
Awali rais Wade alibashiri kupata ushindi mkubwa katika duru ya kwanza ya uchaguzi.
Wakati akipiga kura yake, kiongozi huyo alizomewa na umma mjiniDakar.
Katika mkutano na waandishi wa habari Rais Wade alionekana kutotaka kujibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari.
Aidha raia huyo amesema yuko tayari kuanzisha mazungumzo na upinzani ikiwa kutakuwa na duru ya pili.
Wadadisi wamesema rais Wade atakuwa na kibarua kigumu katika duru ya pili ikiwa upinzani utaungana dhidi yake.
Macky Sall amesema yuko tayari kukabiliana na rais Wade na kuongeza kuwa upinzani umeshinda viti vingi zaidi vya ubunge.
Kiongozi huyo wa upinzani ameelezea imani ya kushinda katika duru ya pili ikiwa upinzani utamuunga mkono.
Senegalimetajwakamamojawapo ya mataifa thabiti zaidi Afrika Magharibi na yenye misingi ya kidemokrasia tangu kupata uhuru wake miaka 60.