TANGAZO


Wednesday, February 15, 2012

Mabingwa wa Afrika walivyolakiwa nyumbani kwao, Zambia

 

Wananchi wakiwa wamejipanga pembezoni mwa barabara kuilaki timu yao nchini Zambia, huku ikisindikizwa na magari ya jeshi.
 
 

Wanajeshi wakiisindikiza timu ya Taifa, wakiwa na kombe la ubingwa wa Afrika walilolitwaa nchini Gabon, baada ya kuifunga Ivory Coast kwa mikwaju ya penalti 8-7.
 
Wananchi wakiishangilia timu ya Taifa, Chipolopolo, ilipowasili na kombe la Ubingwa wa Afrika nchini humo jana.

 
Wananchi wakiwa wamepanda kwenye minara ya Simu, kwa ajili ya kuishuhudia timu yao ya Taifa, ikiwa na kombe la Ubingwa wa Afrika, ilipowasili nchini humo .Mwandishi wa BBC anasema mashabiki waliokuwa wakisubiri, walilipuka kwa kelele za shangwe, wakati nahodha Christopher Katongo alipotoka kwenye ndege akiwa amelibeba Kombe la dhahabu la Mataifa ya Afrika.

No comments:

Post a Comment