TANGAZO


Thursday, February 23, 2012

Katibu Mkuu Hazina afungua mkutano wa Wakaguzi wa hesabu wa ndani

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ramadhan Khijjah akifungua mkutano wa siku tatu wa wakaguzi wa ndani  wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa leo, jijini Dar es salaam, wenye lengo la kuwaelimisha juu ya marekebisho ya Sheria ya Fedha, Sura 348 ya Juni 2010, yaliyopelekea Wizara ya Fedha kuanzisha, Idara ya Mkaguzi wa ndani wa Serikali (Internal Auditor General Division), ambayo pia inajukumu la kusimamia na kuboresha ukaguzi wa ndani kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa na Sekrietarieti za Mikoa. (Picha na Tiganya Vincent, Dar es salaam)


Baadhi ya wakaguzi wa ndani  wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa wakiwa katika mkutano wa siku tatu wenye lengo la kuwaelimisha juu ya marekebisho ya Sheria ya Fedha Sura 348 ya Juni 2010, yaliyopelekea Wizara ya Fedha kuanzisha Idara ya Mkaguzi wa ndani wa Serikali (Internal Auditor General Division), ambayo pia inajukumu kusimamia na kuboresha ukaguzi wa ndani kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa na Sekrietarieti za Mikoa ulianza jana jijini Dar es salaam.


Picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah (wa tatu kulia waliokaa) na baadhi ya wakaguzi wa ndani  wa Sekretarieti za mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa baada ya ufunguaji wa mkutano wa siku tatu wenye lengo kuwaelimisha juu ya marekebisho ya Sheria ya Fedha Sura 348 ya Juni 2010, yaliyopelekea Wizara ya Fedha kuanzisha Idara ya Mkaguzi wa Ndani wa Serikali (Internal Auditor General Division), ambayo pia inajukumu kusimamia na kuboresha ukaguzi wa ndani kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa na Sekrietarieti za Mikoa ulianza jana jijini Dar es salaam.




No comments:

Post a Comment