Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili Lancaster House, jijini London leo February 23, 2012, kwa ajili ya kijiunga na viongozi wa nchi mbalimbali duniani katika mkutano wa kujadili mustakabali wa nchi ya Somalia, ambayo imekuwa katika misukosuko kwa zaidi ya miaka 20 sasa, ambapo Jumuiya ya Kimataifa, ikiongozwa na Uingereza, imepania kumaliza matatizo mbalimbali katika nchi hiyo, ikiwemo kutokuwa na Serikali inayoeleweka, uharamia, ugaidi pamoja na kujaribu kurudisha amani. (Picha na Ikulu)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akielekea kwenye ukumbi wa jengo hilo, ili kijiunga na viongozi wa nchi nyingine duniani katika mkutano wa kujadili mustakabali wa nchi ya Somalia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe (aliyeipa mgongo kamera), wakilakiwa na kukaribishwa kwenye mkutano, unaofanyika jengo la Lancaster House jijini London leo February 23, 2012.
No comments:
Post a Comment