TANGAZO


Thursday, February 23, 2012

Waziri Mbarawa atangaza tarehe ya kusitishwa matangazo ya mfumo wa analogi

 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa, akizungumza na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam, kuhusu usitishwaji wa matangazo ya Televisheni kwa kutumia Technolojia ya analogi na kuhamia teknolojia ya utangazaji ya dijitali, ambao utasitishwa rasmi tarehe 31, Disemba mwaka 2012, saa sita kamili usiku. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo  Dk. Florens Turuka. (Picha na Anna Itenda - Maelezo)


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dk. Florens Turuka akijibu maswali ya waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam kuhusu usitishwaji wa matangazo ya Televisheni kwa kutumia Technolojia ya analogi na kuhamia teknolojia ya utangazaji ya dijitali, ambao utasitishwa rasmi tarehe 31, Disemba mwaka 2012, saa sita kamili usiku. Kushoto ni Waziri wa wizara hiyo Prof. Makame Mbarawa.

No comments:

Post a Comment