TANGAZO


Thursday, February 23, 2012

Makamu wa Rais Dk. Bilal, atembelea kiwanda cha nyama Sumbawanga

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha nyama cha Saafi, mara baada ya kuwasili kwenye kiwandani hapo, kilichopo Wilaya ya Sumbawanga jana Februari 22, 2012, akiwa katika ziara yake ya Mikoa ya Katavi na Rukwa. Kiwanda hicho kinamilikiwa na Mtanzania, Dk. Crisent Mzindakaya (wa pili kulia). (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)


Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu uchinjaji wa Ng’ombe na matayarisho yake hadi kufikia nyama kamili, kutoka kwa Meneja wa  kiwanda cha nyama cha Saafi, Dk. Engelbert Bilashoboka, wakati alipokitembelelea kiwanda hicho, Sumbawanga jana Februari 22, 2012.


 Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipatiwa maelezo kuhusu utayarishaji wa kuchinja ng’ombe na mambo mengine hadi kupatikana nyama kamili kutoka kwa Meneja wa  Kiwanda cha Nyama cha Saafi, Dk. Engelbert Bilashoboka.


 Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipatiwa maelezo kuhusu vipimo vinavyotumika kabla ya  ng’ombe kuchinjwa kutoka kwa Meneja wa  kiwanda cha nyama cha Saafi, Dk. Engelbert Bilashoboka.


Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu matayarisho na ufungaji wa nyama katika mifuko, tayari kwa kuuzwa kwa wateja kutoka kwa Meneja huyo.

No comments:

Post a Comment