Mbunge wa Same Mashariki Anna Kilango akijadili jambo na Mwanasheria mkuu wa serikali Jaji Frederick Werema ndani ya ukumbi wa Bunge leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu mjini Dodoma.
Mbunge wa Singida Mjini, Mohammed Dewji, akimsikiliza kwa makini Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira ndani ya ukumbi wa Bunge leo, mjini Dodoma.
Mbunge wa Bumbuli, January Makamba, akiwasilisha Hoja binafsi, kuhusu Sheria ya udhibiti wa shughuli za upangaji nyumba za makazi, aliyoitoa chini ya kanuni ya 54 (1) ya kanuni za bunge, toleo la 2007, ya kuliomba Bunge kuazimia kwa kauli moja, kuitaka Serikali katika mkutano ujao wa Saba, kuleta Muswaada wa Sheria ya kudhibiti Upangaji wa Nyumba na Makazi kufuatia malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wanaoishi mijini kutokana na adha wanazozipata katika kutafuta nyumba za kupanga au kuishi.
No comments:
Post a Comment