Makamu wa Rais wa kundi la Akudo Impact, Tarsis Masela (JOTO), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akiwatambulisha waimbaji watatu wapya, waliojiunga na bendi hiyo, wakitokea nchini Zaire. Kushoto ni mmoja wa waimbaji hao, J. Love aliyekuwa kwenye kundi la JB Mpiana wa nchi hiyo. (Picha na Kassim Mbarouk)
Tarsis Masela (JOTO), akimtambulisha mwimbaji Blavier Katoto, aliyekuwa na kundi la Feli Ipupa la Zaire, ambaye amejiunga na kundi la Akudo.
Waimbaji wapya wa kundi la Akudo, kutoka kushoto waliosimama, J.Love, Blavier Katoto na Fabrice-Mombili 'Mulia-lia', waliowasili nchini na kujiunga na kundi la Akudo impact hivi karibuni wakiimba wimbo wao mpya walioutunga kwa ajili ya kundi lao hilo jipya, unaoitwa Ferre-Gola. Waliokaa katikati ni Makamu wa Rais wa Akudo, Tarsis Masela (kushoto) na mpiga gitaa la Solo, Merle-Solo-Yamba.
Hapa wakiimba wimbo wa bendi yao mpya, unaoitwa Walimwengu si Binadamu, wakati wa utambulisho huo, ambao wataanza kuonekana kwenye jukwaa, keshokutwa Ijumaa, wakifanya vitu vyao, ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar es Salaam. (Picha na Kassim Mbarouk)
No comments:
Post a Comment