Kisa hicho kimetokea siku chache tu baada ya serikali zote mbili kutia saini mkataba wa kusitisha uhasama kati yao mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Jamhuri ya Sudan bado haijatoa taarifa kuhusu tukio hilo.
Mji wa Jau ambao upo kwenye mpaka wa jimbo la Unity na lile la Kordofan kusini, umekuwa ukizozaniwa na serikali zote mbili.
Msemaji wa Jeshi la Sudan Kusini ameongeza kuwa wanajeshi wa serikali ya Khartoum wameongezwa kwenye mipaka yao karibu na mji huo.
Wanajeshi wa Jamhuri ya Sudan wamekuwa wakikabiliana na waasi wa kundi la SPLM-North ambao wanadai kuwa wanapata usaidizi kutoka wa serikali ya Sudan Kusini.
Hata hivyo utawala mjini Juba umekanusha madai hayo mara kadhaa.
Wadadisi wanasema ikiwa shambulio hilo litadhibitishwa, huenda likachochea uhasama zaidi kati ya majirani hao wawili.
Ijumaa iliopita wawakilishi wa serikali hizo walikubaliana kusitisha uhasama kati yao uliozuka baada ya mzozo kuhusu kusafirisha mafuta kutoka Sudan Kusini hadi kwenye bandari ilioko Khartoum.
No comments:
Post a Comment