TANGAZO


Wednesday, February 15, 2012

Kili Marathon kufanyika Februari 26, 2012, Mjini Moshi

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Executive Solution, Aggrey Marealle, ambao ni waratibu wa mbio hizo, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu mbio za Kili Marathon, zilizoandaliwa na Kampuni ya Wild Frontiers ya Afrika Kusini, zitakazofanyika Februari 26, mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro. Kulia ni Mkuu wa Udhamini wa Kampuni ya Simu ya Vodacom Tanzania, ambao ni moja ya kampuni, wadhamini wa mbio hizo, Ibrahim Kaude. (Picha na Kassim Mbarouk)


 Mkurugenzi wa Kampuni ya Executive Solution, Aggrey Marealle, ambao ni waratibu wa mbio hizo, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika mkutano huo. Kulia ni Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania, Ibrahim Kaude, Rais wa Chama cha Riadhaa Tanzania (TAA),  Francis John (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Julias Musomi.


Rais wa Chama cha Riadhaa Tanzania (TAA), Francis John, akizungumza katika mkutano huo, kuelezea ushiriki wa wanariadha maarufu wa ndani na nje ya nchi, kwenye mbio hizo. Watatu ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Executive Solution, waratubu wa mbio hizo, zilizoandaliwa na  Kampuni ya Wild Frontiers ya Afrika Kusini, Aggrey Marealle.

No comments:

Post a Comment