Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bi. Amina Mafita akizungumza na wadau wa Ustawi wa Jamii Jijini Dodoma wakati akifungua kikao kati ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Wadau kujadili utekelezaji wa Mpango Mkakati wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto nchini.(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW)
Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi akizungumzia lengo la kikao kati ya Wizara na wadau Jijini Dodoma wakati wakijadili utekelezaji wa Mpango Mkakati wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto nchini.
Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Filbert Kawemama akizungumza kuhusu utekelezaji wa Mpango Mkakati wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto nchini kwa upande wa wizara kwa wadau wa Ustawi wa Jamii Jijini Dodoma.
Mwakilishi kutoka Shirika la WELD EDUCATION Bi. Grace Muro akielezea utekelezaji wa Mpango Mkakati wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto nchini kwa upande wa Shirika lake katika kutokomeza vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wakati walipokutana na Serikali kujadiliana kuhusu utekelezaji wa mpango huo.
Mwakilishi kutoka Shirika la IMO Bi. Gracia Anthony akielezea utekelezaji wa kwa upande wa Shirika lake katika kutokomeza vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto nchini wakati waliokutana na Serikali kujadiliana kuhusu utekelezaji wa Mpango Mkakati wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto nchini.
Mwakilishi kutoka Shirika la JSI Bw. Anthony Mwendamaka akielezea utekelezaji wa kwa upande wa Shirika lake katika kutokomeza vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto nchini wakati waliokutana na Serikali kujadiliana kuhusu utekelezaji wa Mpango Mkakati wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto nchini. Baadhi ya wajumbe wa kikao kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinisia, Wazee na Watoto na wadau wa Maendeleo wakifuatilia maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na Serikali pamoja na wadau wa Ustawi wa Jamii katika utekelezaji wa Mpango Mkakati wa kutomomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto nchini.
VIDEO
Na Mwandishi Wetu -Dodoma
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto leo imekutana na wadau wa maendeleo kujadili hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa Mpango mkakati wa kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto hususani eneo la sita la mkakati huo linalohusiana na eneo la huduma kwa waathirika wa ukatili na unyanyasaji wa watoto nchini.
Wizara kupitia idara ya Ustawi wa Jamii ina jukumu la kusimamia Mpango Mkakati wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na watoto eneo la sita la kukabili vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto hivyo leo imeitisha kikao na wadau wa maendeleo kama hatua ya utekelezaji wa eneo hilo la mkakati.
Akizungumza katika kikao hicho Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bi. Amina Mafita amewaambia wajumbe wa kikao hicho kuwa wanakutana kujulishana na kupeana taarifa kuhusu hatua za utekelezaji wa mpango mkakati huo katika juhudi za kutokomeza vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi ya watoto kama ilivyo kwenye eneo la sita la mkakati huo.
Aidha Bi. Amina ameongeza kuwa baadhi ya Mashirika yanayotekeleza eneo la sita la Mkakati wa Kutomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto yatatakiwa kuonesha na kuwataarifu mashirika mengine ya wadau wa maendeleo kuhusu maeneo yanayayofanyia kazi katika ngazi ya Mkoa, Wilaya mpaka Kijiji.
Ameyataja maeneo muhimu yakufanyia kazi kwa baadae kuwa ni kupunguza idadi ya watoto wa mitaani, ajira kwa watoto katika mkakati utakaohusisha familia lakini pia kuandaa mwongozo wa uanzishaji wa makazi salama ya watoto ambao ni waanga wa ukatili.
Mpango Mkakati wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto una maeneo nane ya utekelezaji mojawapo ni eneo la sita linalohusiana na kukabiliana na vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto na kutoa huduma kwa waathirika wa ukatili na unyanyasaji wa watoto utekelezaji wa mapango huu ni wa kipindi cha miaka mitano 2017/2018-2021/2022.
No comments:
Post a Comment